ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, January 2, 2016

BREAKING NEWS,MWIGULU NCHEMBA ATIMUA KIGOGO WA KUIBA USHURU WA MIFUGO-PUGU,AWASHIRIKISHA MAWAZIRI 3 KUSAFISHA MACHINJIO YA VINGUNGUTI

FMh:Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh:Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh:Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mh:Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mh:Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.Mh:Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mh:Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.
 
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais J.Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.
Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.
Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.
 
Picha/Maelezo na Festo Sanga

3 comments:

Unknown said...

Inatia furaha kuona uwajibikaji uliotukuka ukitekelwasipoyapata maendeleo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM ila aliendelea kusema tunapokuja kumtafuta raisi bora wa kuingoza nchi yetu katika maendeleo ya kweli basi raisi bora huyo lazima atoke ndani ya CCM. Na dhani hata ukawa waliibeba kauli mbiu hiyo ya mwalimu kwa kumsimamisha mwana CCM kuwa mgombea wao wa uraisi isipokuwa walimteuwa mtu sie. Don't get me wrong upinzani Tanzania wanastahiki pogezi sijui bila ya upizani nchi yetu ingekuwa ipo katika hali gani. Ninacho kiona upizani walikosa elimu bora ya upizani kitu ambacho kilipelekea kupoteza mwelekeo baadae sijui kutokana na shinikizo la chama tawala au uduni wa elimu ndani ya watendaji wa upizani. Sina ufahamu na viwango vya elimu vya watu wa upizani lakini CCM licha ya ufisadi wao wao kile chama kimejaa wasomi na mungu bariki watanzania wamemuweka madarakani msomi wa kiwango cha juu na anachokifanya sasa ni kuwakumbuka wasomi wenzake kwa kuwapa nafasi za uongozi sio wanasiasa kama ilivyozoeleka katika awamu zilizopita.kwa upande wa upizani hawana haja kujitia unyonge na kujiweka mbali na serikali wanatakiwa kusahau yaliyopita na kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita. Kama kuna kitu waafrica tunamatatizo nacho basi kukubali na kutamka hadharani kwa roho safi kabisa kuwa umeshindwa hata kama kweli tumedundwa vilivyo basi lazima tutakuwa na visingizio hata kama kusingizia uchawi. Sifikirii kama watanzania wengi wanafahamu kuwa uchaguzi kati ya George Bush na Algore ulikuwa na utata wa kisawa sawa licha ya kwamba Bush kutangazwa kuwa raisi. Vile vile uchaguzi kati ya John Kerry na George Bush zengwe heavy tu. Lakini licha ya kasoro zote zilizojitokeza katika chaguzi hizo za marekani mara baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza George Bush kuwa mshindi kilichofuatia ni kwa Algore na John Kerry kunyanyua simu na kumpongeza raisi mtarajiwa Bush. Sasa leo bado tunamuona lowasa akiendelea kuteseka mara kanisani,mara msituni akikimbiza ng'ombe mara maandamano wakati kuna kitu kidogo tu angekifanya ambacho kingemletea peace kwenye roho yake na heshima pengine kuliko hata kwenda kuungama kanisani ni kunyanyua simu na kumpongeza mpinzani wake kwa kuchaguliwa kuwa raisi that's all. lakini tusishangae hiyo ni tofauti yetu sisi waafrika na hawa watu tunaowaita wazungu kwa maana halisi ya mzungu kwa tafsiri ya kiswahili ni kitu cha ajabu na wacha tuwaone wazungu watu wa ajabu wakati wao wakitusjabia sisi na ujinga wetu wa kuwaona wao watu wa ajabu. Mchakato wowote wa kumtafuta mshindi katika ya washindani lazima utakuwa na changamoto zake lakini inapotokezea ushindani huo kuwa wa malengo mamoja ya kuboresha taasisi husika na kwa bahati nzuri katika ushindani huo akipatikana mtu sahihi wa kazi tena ubinafsi wa nini? Wakati wote mna malengo ya kuboresha mjengo ya nini kugombania fito wakati mjenzi sahihi keshapatikana. Tunataka upizani uwe na nguvu Tanzania daima lakini upinzani huo kama utakuwa hauweki maslahi ya taifa kwanza basi utakuwa hauna faida yeyote. Kazi anayoindelenayo mueshimiwa raisi ni ya kuvutiya na kupongozwa kiasi kwamba waafrica wote wenye kutaka kuliona bara la Africa likipiga hatua kimaendeleo wamethubutu kusema kama maghufuli angelikuwa mchezaji wa mpira wangelifanya vyovyote iwezekanavyo wamsajili ili awaletee mabadiliko katika timu zao.Sasa nakaa nikijiuliza kipi kilichokuwa kinatafutwa na akina Mbowe na genge lake ni upinzani wa kulipeleka taifa katika maendeleo ya kweli na kuondokana ufisadi na ubadhirifu na uozo wa kila aina uliokuwa umekithiri na kuliondoa taifa katika umasikini au upinzani wa kujitafutia maslahi binafsi na ya chama kwanza na nchi baadae? Kama akina Mbowe na genge lake wanauchungu na Tanzania na kuweka maslahi ya wananchi kwanza wanatakiwa kuunga mkono jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya muheshimiwa Magufuli tena wafanye hivyo haraka sana, la kama wanauchungu wa chadema na maslahi yao wao wenyewe binafsi basi watanzania si wapumbavu.

Anonymous said...

chapeni kazi vijana and you have my support, msisikie la mjinga yoyote.

Anonymous said...

Wapi na wapi watu wa sera wakawa ndio hao hao wa utekelezaji wa sera hizo hizo. Nchi inatakiwa kuendeshwa kwa mfumo si hizi sinema za kina Mwigulu, Deputy Minister afya nk. Huu upuuzi tu kama si nguvu mpya, ari mpya na ...mpya tu za jk au askari wa miavuli wa nkapa