Wednesday, January 13, 2016

CCM yaomba radhi

Mkuu wa Mawasiliano na Umma wa CCM, Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma wa CCM, Daniel Chongolo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi, ulioandikwa kwenye moja ya mabango lililobebwa na mmoja wa wananchi, waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar, jana.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mawasiliano na Umma wa CCM, Daniel Chongolo, jijini Dar es Salaam jana, ilisema Chama cha Mapinduzi kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

“Ujumbe huo, sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi, bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza umoja na mshikamano wa Kitaifa,” ilisema taarifa hiyo.

HABARI LEO

8 comments:

Anonymous said...

Mbona CCM zanzibar Haijaongea chochote kuhusu ujumbe huo wa kibaguzi, pengine ndio sera ya sasa ya CCM Zanzibar.

Anonymous said...

Hata bado hamjaadhirika mwaka huu mulisoma dua ya pamoja na ubani mukatia kuiombea znz .dua inawarejea wenyewe munajifanya waungu watu .angalia sasa mumeshindwa kumtangaza mshindi kimya CUF wabaguzi kumbe nyie wenyewe tangu kisonge mpaka amani na viongozi wenu kimya lkn jueni znz ikichafuka mujue la kujibu hamtaishi milele na kila mtu atazikwa peke yake sasa kama mnaringia jeshi juilezeni litaishia wapi cku pumzi itakapomaliza

Anonymous said...

Hiyo sera yao ya zamani walikua wakiwafanya wazenji wajinga kumbe wajinga wenyewe wanaowatakia mema hawawajui wamebaki na ufinyu wa maneno poleni sana wa znz kwa viongozi wenu mliowachagua kichama sio kimaendeleo visiwa havizidi watu milioni vinanuka njia wametunyonya mpaka magaga poleni machora wa ccm kumbe mnapakwa mafuta tu dah! Poleni sana

Unknown said...

WACHENI FITINA HIZI NDO SERA ZA CCM HUSUSA ZNZ MBONA HAMJA LINGOWA BANGO LA KISONGE , HII MOJA YA ITIKADI ZA SISI EMU KUMBUKENI WAZIRI WA CCM ALIVYO SEMA KUHUSU ZNZ, NA JUU YA WAISLAMU, KUMBUKENI CCM WALIVYO WAFANYA MASHEHE , LIKA SEREKALI KUKE MEYA, ILOOOOO MSOHAYA ELOOO,

Anonymous said...

HAPA CCM KAMA WANAKUNYA NA KUJPAKA MAVI WENYEWE, HII SERA YA UBAGUZI IPO NA ITAENDELEA KUWEPO, TANGU MAPINDUZI YA 1964 YALIOIPINDUA SERIKALI HALALI ILIOCHAGULIWA NA WANANCHI DECEMBER 9, 1963, CHUKI ILIANZA KUMEA NA INAENDELEZWA MPAKA LEO, MAPINDUZI IMEKUWA NI SLOGAN YA CCM KWAMBA TUMEJIKOMBOA KUTOKA KATIKA MIKONO YA WAKOLONI, UKWELI ZANZIBAR ILIKUWA CHINI YA MTAWALA MWEUSI MAREHEMU MOHAMED SHAMTE MUAFRIKA MWEUSI ALIECHAGULIWA 1963 BAADA YA UCHAGUZI HURU, KARIBU VINGOZI WOTE WALIO WAHI KUINGOZA ZANZIBAR WALITAWALA NA KUENDELEZA SERA HII YA UBAGUZI, IPO MIFANO MINGI TU JINSI CCM NA WATAWALA WAKE WANAVYO WAGAWA WANANCHI KWA UKABILA NA MAENEO WANAYOTOKA, SALIM AHMED SALIM ALIIKOSA NAFASI YA URAISI 1985 DAKIKA YA MWISHO BAADA YA WAHAFIDHINA WA ZANZBAR KUPINGA NAFASI HIYO KUPEWA KWA RANGI YAKE NA ALIKOTOKA, UTAWALA WA SALIMINI AOUR NDIO ULIOKUWA MBAYA ZAIDI KATIKA HISTORIA YA UBAGUZI WA ZANZIBAR, BADDA YA UCGAGUZI WA 1995 WAPEMBA WOTE NA WENYE ASILI YA UCHOTARA WALIODHANI TU WALIWAUNGA MKONO WAPINZANI WALIFUKUZWA KAZI, NA WIZARA YA FEDHA NDIO ILIOONGOZA KWA KUWAFUKUZA KAZI WAPEMBA IKIWA CHINI YA WAZIRI AMINA SALIM ALI, WAKATI HUO AKIWA WAZIRI KIONGOZI GHARIB BILAL AKIHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA UWANJA WA FARASI KIJANGWANI ZANZIBAR ALIWATAKA WAUNGUJA WOTE WAITUMIE FURSA YA KUSOMA NA SERIKALI IKO PAMOJA NA WAO KUHAKIKISHA KILA MUUNGUJA APTIWE NAFASI YA KUSOMA.
BORAFYA KAMA MWENYEKITI WA CCM MKOA WA NJINI MAGHARIBI MAESHATUKANA MARA NGAPI NA SPEECH ZAKE IKIRUSHWA KATIKA TV ZANZIBAR HAKUNA ALIEKEMEA, SALIMIN AMOUR ALIWATISHA WAPEMBA BAADA YA UCHAGUZI WA 1995 WAKAWA WANAONDOKA KURUDI PEMBA, BAADA YA KUONA WIMBI LA WAHAMAJI LINAONGEZEKA, POLISI WAKWA WANAWAZUIYA WATU KUSAFIRI WAKIWAONA WANA MIZIGO, WALIKUWA HAWAWARUHUSU KINGIA BANDARINI, HUU WOTE NI UBAGUZI UNAOFANYA NA CCM, KUNA MATOKEO MENGI, MENGI TU, HAPA NAWEKA KWA UFUPI TU.

Anonymous said...

Kwani kuzungumza ukweli kuna tatizo gani na ndio maana CCM Zanzibar haito omba radhi kwa huo ujume unaolalamikiwa kuwa wa kibaguzi. Zanzibar ipo Africa na wamiliki halali wa Zanzibar ni wanzanzibar wanaojitambua kuwa wao ni waafrica na yeyote anaejinasibu kuwa yeye ni mwarabu alafu anafurahia kwa kusema seifu akishinda ni ukombozi wa wazanzibari? Ni wazanzibari gani tena hao? Na hapo ndipo inapowapelekea wazanzibari halisi watoke na mabango wenye ujumbe wa wamubukusha wapuuzi kuwa Zanzibar ina wenyewe na ni kweli kabisa ya kwamba Zanzibar ina wenyewe na wenyewe. Vile vile mapinduzi ya Zanzibar yamefanyika baada ya unyanyasaji ulipitiliza mipaka kwa wazanzibari weusi. Kati ya wazanzibari walisha ridhia kuwa third class citizen maisha yao yote kutokana na misingi haramu ya kitabaka iliokwisha ota mizizi kwa muda mrefu. Kuna waliojiita waarabu wakati ukimkuta mjodani anakwambiwa wamisri sio warabu na hata wakiongea hawaelewi wanaongea lugha gani. Sasa wamisri sio waarabu wewe mpemba au mzanzibar uwarabu umeupata wapi? na kama si ugonjwa wa akili kitu gani? Huyo Mohamed shamte anaedaiwa kupinduliwa ni kibaraka aliekuwa yupo tayari kula kinyesi cha waarabu ilimradi kuhakikisha wazanzibari wanakuwa chini ya utawala wa kisultani.Na kwa kuweka history ya Zanzibar sawa bila ya kupotoshwa, aliepinduliwa katika mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 si Mohammed shamte bali ni serikali ya kisultani iliokuwa chini ya mtawala wake aliejulikana kwa jina la Jamshid bin Abdullah, huyo Mohammed shamte alikuwa mpambe wa kujipendekeza kwa wakoloni kama unavyomuona maalimu seif.

Anonymous said...

KIU KWERI KWENYE HILI, MUWE WA KWERI KWA (MUSTAKABALI) WA ZANZIBAR.

.FUTURE YA ZANZIBAR. ANGALIA HAPA KWENYE YOUTUBE"
Sultan Jamshid Sultani of Zanzibar.

Anonymous said...

Ccm wabaguzi mno. Tunamtaka maalimu seif.