ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 6, 2016

KUSUDIO LA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI YANAYOJIENDESHA KINYUME CHA SHERIA



    TAARIFA KWA UMMA


Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali tanzania anakusudia kuyachukulia hatua Mashirika yanayoendesha shughuli zao kinyume cha Sheria ya NGOs Na. 24 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005.


Taarifa iliyotolewa leo na ofisi hiyo imesema mashirika hayo ni yale ambayo hayajawasilisha taarifa za mwaka kwa kipindi cha miaka miwili pasipo kutoa sababu za msingi, kulipa ada ya mwaka au kuendesha shughuli za NGOs bila kusajiliwa chini ya Sheria ya NGOs.


Kwa taarifa hii, Mashirika husika yanatakiwa yawe yamerekebisha dosari tajwa ndani ya siku thelathini (30) kuanzia tarehe ya tangazo hili. Baada ya kipindi hicho, Msajili wa NGOs atayafutia usajili.


Mashirika ambayo yatakuwa hayajawasilisha taarifa na kuyachukulia hatua stahiki Mashirika yanayoendesha shughuli za NGOs bila ya usajili chini ya Sheria husika.


Malipo yote ya ada yafanyike kupitia Benki ya NMB, NGO Account Na. 20110014074 na stakabadhi halali ya malipo itumwe kwa Msajili wa NGOs.

Imetolewa na:

M.S. Katemba
MSAJILI WA NGOs
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII,
JINSIA, WAZEE NA WATOTO
06 Januari, 2015

No comments: