Dar es Salaam. Mwili wa kijana, Abel Machanga (24), aliyefariki dunia Desemba 31, mwaka jana katika Hospitali ya Colombia Asia, India umekwama baada ya ndugu wa marehemu kukosa fedha za kulipa deni la Sh35 milioni wanazodaiwa na hospitali hiyo.
Takribani siku 27 zimekatika tangu kijana huyo afariki na kwa muda wote huo, baba yake; Revocatus Machanga amekuwa akihaha kuomba msaada. Abel alifariki dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao tangu 2015 na Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi yake hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 za Marekani zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India. Mara baada ya kufika India na kufanyiwa vipimo, uongozi wa hospitali hiyo ulitaka kuongezewa dola 5,000. “Tulijichangisha nikatuma fedha hizo matibabu yakaanza.
Novemba 30 mwaka jana, alifanyiwa upasuaji alipokuwa bado kwenye uangalizi waligundua kuwa ana degedege, bakteria karibu kila sehemu ya mwili wake na shinikizo la damu kushuka kupita kiasi,” alisema na kuongeza wakati wakiendelea kumhudumia, waligundua maradhi mengine hivyo kudai kuongezewa dola 16,396 sawa na Sh35milioni.
“Nilikwenda Wizara ya Afya kuomba msaada, waliniahidi kuna taarifa walimuagiza mwambata wao aliyekuwa India kufuatilia.
Msemaji wa Wizara ya Afya, Nsachris Mwamaja alisema hana taarifa kuhusu suala hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi wa kina leo.
No comments:
Post a Comment