Habari zilizopatikana kutoka mjini Mpanda zinasema mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda mkoani Mara na baadhi ya marafiki zake walioshirikiana na Chama cha Wenyeji wa Mara waishio mkoani Katavi.
Katavi. Jeshi la Polisi mkoani Katavi limegoma kuusafirisha mwili wa askari Nobert Chacha (25) aliyeuawa kwa kupigwa risasi kifuani katika tukio la ujambazi nyumbani kwa mfanyabiashara wa madini.
Habari zilizopatikana kutoka mjini Mpanda zinasema mwili wa marehemu ulisafirishwa jana kwenda mkoani Mara na baadhi ya marafiki zake walioshirikiana na Chama cha Wenyeji wa Mara waishio mkoani Katavi.
Mjumbe wa chama hicho, Julius Marwa alisema walilazimika kusafirisha mwili huo baada ya Polisi kukataa kuusafirisha kwa madai kuwa kitendo alichofanya askari huo tayari alikuwa amejifukuzisha kazi.
Kamanda wa polisi mkoani humo, Dhahiri Kidavashari alisema kwa taratibu za jeshi, mwili huo haukustahili kupewa heshima yoyote, ikiwa ni pamoja na kusafirishwa kwa kuwa ni aibu na fedheha kutokana na kitendo alichofanya.
Askari huyo wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda aliuawa wakati wa usiku akiwa katika harakati za kuiba kwa kutumia silaha za jadi nyumbani kwa mfanyabiashara huyo anayejulikana kwa jina la Daniel John.
Tukio hilo lilitokea kwenye Kijiji cha Ibindi kilichopo Kata ya Machimboni wilayani Mlele. Mfanyabiashara huyo alimpiga risasi ya kifuani askari huyo aliyekuwa na wenzake ambao idadi yao haijajulikana.
Diwani wa kata hiyo, Raphael Kalinga alisema askari huyo akiwa na wenzake walifika kijijini hapo kwa nia ya kumpora mfanyabiashara mali zake.
Inadaiwa walivunja mlango na kuingia ndani ya nyumba, kisha walimwamuru kukaa kimya, lakini hakutii agizo hilo na badala yake alichukua bunduki yake aina ya shortgun na kufyatua risasi ambayo ilimpiga askari huyo sehemu ya kifuani na mgongoni na kufa papo hapo.
No comments:
Post a Comment