Monday, January 18, 2016

SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA YA SEBO KUTOKA KWA BALOZI LIBERATA MULAMULA


Balozi Liberata Mulamula akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 37, ya CCM  yaliyofanyika College Park katika hotel ya Hampton INN Feb 23, 2014 wakati huo Balozi Mulamula akiwa balozi wa Tanzania nchini Marekani. Kushoto ni marehemu George Sebo ambaye alikua mwenyekiti wa CCM DMV mpaka leo siku ya Jumatatu January 18, 2016 alipokutwa na mautio katika hospitali ya Prince Geoge iliyopo Maryland nchini Marekani.

Nimepokea taarifa ya msiba wa Mzee George Sebo kwa mstuko na huzuni kubwa. Naomba kuwapa pole wana jumuiya wote na wanachama wa CCM DMV kwa msiba huo mkubwa sana. Naomba munifikishie salaaam zangu za rambirambi kwa mkewe Mama Grace Sebo na wanafamilia. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake ya upendo mahali pema peponi. Bwana ametoa, Bwana amechukua, jina lake lihidimiwe.


Awakumbukaye daima,

Balozi Liberata Mulamula
Dar es Salaam
Tanzania

No comments: