Advertisements

Sunday, February 14, 2016

JINSI MITUME NA WANAFUNZI WA YESU KRISTO WALIVYOKUFA.

1. Mathayo.
Huyu aliuawa kwa upanga baada ya kuonyesha imani kali dhidi ya kanisa la kristo.

2. Marco
Huyu alifariki huko Alexandria Misri ya sasa baada ya kuangushwana farasi barabarani, aliangushwa vibaya na hakupata msada. Mwishoe alifariki.

3. Luka
Alinyongwa huko Ugiriki, hii ni kutokana nà msimamo wake mkali aliouonesha dhidi ya kristo.

4. Yohana
Huyu alitumbukizwa katika pipa lenye mafuta yanayochemka huko Roma, Italia ya sasa. Hata hivyo kwa miujiza hakuungua na alitolewa akiwa mzima kabisa. Alipelekwa katika gereza lililokuwa katika migodi huko kisiwa cha Patmos. Na huko ndiko alipofunuliwa na mwenyezi Mungu na kuandika kitabu cha "Ufunuo wa Yohana". Baadae aliachiwa huru na kwenda kutumika kama askofu huko Edessa Uturuki ya sasa. Alifariki akiwa mzee sana. Na ni mtume pekee aliuefariki bila mateso.

5. Petro
Huyu alipata adhabu ya kifo cha msalaba. Ila yeye alisurubiwa tofauti na Yesu kristo. Kusurubiwa kwa Petro ilikuwa kichwa chini miguu juu katika msalaba. Hii ni kwa ombi lake yeye mwényéwé hakutaka kusurubiwa kama Yesu.

6. James
Alikuwa Kiongozi wa kanisa huko Jerusalemu Israel ya sasa. Yeye alitupwa kutoka juu kabisa ya mnara wa hekalu wenye urefu wa meta 100 baada ya kugoma kumpinga kristo (mnara huo ni kama ule ambao shetani alimjaribu Yesu kwa kumwambia kama yeye ni mwana wa Mungu ajirushe). Walipogundua kuwa hajafa baada ya kumdondosha tokea juu ya mnara, maadui walimpiga na mawe mpaka akafa.

7. James mwana wa Zebedayo
Alikuwa ni mvuvi kabla Yesu hajamteua kuwa mwanafunzi wake. Akiwa kiongozi mkubwa wa kanisa, James alichinjwa huko Jerusalemu. Maajabu ni kwamba askar aliyekuwa akimlinda gerezani alishikwa ba mshangao jinsi James alivyoshikiria msimamo wake wa kanisa wakati wa hukumu. Baadae yule askari alienda akapiga magoti mbele ya James na kikiri imani yake mpya juu ya kristo. Wote walichinjwa mbele ya kadamnasi ya watu.

8. Bartholomeo
Pia alijulikana kama Nathanieli. Alikuwa ni mmisionari huko Asia ya sasa. Alimshuhudia Yesu kristo huko Uturuki. Yeye aliuawa baada ya kugoma kuacha mafundisho yake ya kanisa.

9. Andrea
Aliuawa kama Petro. Kifo cha msalama miguu juu kichwa chini. Ila maajabu baada ya kuwambwa msalabani aliendelea kupaza sauti akihubiri neno la Mungu mpaka mauti ilipomchukua.

10. Thomasi
Aliuwa kwa kupigwa na mshale huko India ya sasa.

11. Yuda (sio eskariote)
Nae pia alipigwa na mshale.

12. Mathias
Mwanafunzi aliyeteuliwa na Yesu kuziba nafasi ya Yuda eskariote msaliti. Huyu alipigwa na mawe hadi kufa na baada ya hapo walimkata kichwa.

13. Paulo
Aliteswa na baadae akachinjwa na Emperor Nero huko Roma mwaka 67 Ano Domino (A.D). Paulo aliishi muda mrefu sana gerezani ambapo akiwa huko aliandika barua(waraka) nyingi kwa makanisa ya Roma. Ndio hizi ambazo zinafundisha misingi ya ukristo katika agano jipya, kama vile Waraka wa Paulo mtume kwa Warumi, Wakoritho, Waefeso, Wakolosai, Wathesalonike, Timotheo etc.

Inawezekana hii ni kumbusho kwetu kwamba mateso tunayopitia ni madogo sana ukiringanisha na haya ambayo mitume waliyapitia. Yote ni kwa ajili ya kutetea kanisa la Mungu. Ajabu siku hizi watu wamegeuza dini ya kikristo kuwa sehemu ya upigaji wa hela kutoka kwa masikini!

"Nanyi mtakuwa mkichukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu, lakini mwenye kuvumilia mpaka mwisho, ndiye atakayeokoka." Mathayo Mtakatifu 10:22

Alex Ferdinand Mfikwa

7 comments:

Anonymous said...

Mr alex Ferdinand mfikwa Asante kwa somo lako ninachoomba kutoka kwako ni ushahidi wa hayo uliyoandika umeyatoa katika maandiko matakatifu? Wapi chanzo cha habari yako ilitusijisema wanena kwa matamanio yako, mwisho Paulo akuwa mwanafunzi

Bishop Melchizedek said...

Napongeza maelezo mazuri hapo juu lakini napenda wasomaji elewe kuwa kifo cha Mathayo na Luka have kutokana na wao kupinga Imani ya kikristo Bali kwa kuisimamia Imani hio bila kutetereka. Nadhani maandishi amtumie neno .."dhidi".kimakosa.

Thanks.

Anonymous said...

Mtoa Maoni wa kwanza, soma kichwa cha Habari, Alex amesema kwamba " Jinsi Mitume na Wanafunzi" hivyo wewe unatakiwa kujua kama Paulo alikuwa mtume au mwanafunzi.

Anonymous said...

Kumbe ukristu sio kazi ndogo.Mungu akubariki kwa taarifa hizi zitatusaidia wengi. asante.

Anonymous said...

Swali alilouliza anonymous wa kwanza ni wapi chanzo cha habari? na anajua kama paolo ni nani? ndio maana akasema akuwa mwanafunzi jibu litatusaidia wengi kufahamu maandiko na historia ya kanisa malumbano nadhani hapa sio Mahala pake

Unknown said...

Barikiwa sana.

Ni kielelezo tosha cha kukuza imani yetu juu ya Kristo.

Unknown said...

Barikiwa sana.

Ni kielelezo tosha cha kukuza imani yetu