ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 25, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu Feb 22 2015. SIKU 100 ZA MAGUFULI

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania yetu ya sasa na ile tuitakayo

Katika kipindi hiki utasikia mjadala kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya 5 katika siku 100 za mwanzo

1 comment:

Anonymous said...

Nachukua nafasi hii tena ya kupongeza uwepo wa hiki kipindi kizuri tu ila malalamiko yangu na nafikiri sio malalamiko yangu bali ya wasikilizaji wengi wanafuatilia hiki kipindi ni kuhusiana na kurejea tena na tena kusikiliza maelezo au malalamiko ya upande mmoja ya ndugu Libe unajua kwa kiasi fulani inakera sana kwa sababu kwa sisi tulioishi huku nje kwa muda mrefu tumeshazoea kuona fairness katika masuala ya habari hasa za kisiasa kwamba wahusika fulani wa kisiasa katika mkanganyiko wa jambo fulani lazima wote wawe na nafasi sawa za kutoa maoni yao na yatakapokosekana maoni ya mmoja ya wahusika hao wawili na kupelekea kusikiliza one side story tunazichukulia hizo habari ni za uzushi mtupu. La kushangaza zaidi yeye brother Libe anajiita ni mwanamabadiliko na anatoka katika nchi ambayo anajua kabisa yakwamba kama Hilary Clinton atatakiwa kutoa maoni kuhusu Bernie Sanders basi na Bernie Sanders vile vile atapewa nafasi ya kumjibu Hilary katika wakati sawa. Sasa tumekuwa tukimsikiliza brother Libe akitoa malalamiko yake bila ya kupata maoni ya upande mwengine nafikiria hii sio haki hata kidogo na hatujali yakuwa ni mwanadiaspora na kila anachokisema tukiamini kuwa ni cha ukweli kwanza tayari yeye ameshajiingiza kwenye siasa kwa hivyo ni mwanasiasa na wanasiasa siku zote ni watu kupindisha ukweli na ndio maana watu wanashindwa kufahamu yakuwa Maghufuli sio mwanasiasa na ndicho kitu kimoja ambacho kimekuwa kikimtofautisha kati yake yeye na viongozi wengine na hapana shaka magufuli na serikali yake watafanikiwa. Maghufuli ana miezi mitatu leo watu washaanza kulalamika ati kawaachia wasiolipa kodi bila ya kuwachuchukulia hatua, jamani? Taratibu anazochokuwa magufuli za wafanyabiashara wasiolipa kodi ndizo taratibu ambazo tumeziona zikichukuliwa hata hapa marekani kwanza kabisa mhusika anatakiwa kulipa kodi anayodaiwa na serikali na faini ikiwezekana huku taratibu za kimahakama zikifuata katika kukamilisha taratibu za kisheria. Cha kushangaza watu haohao wanaosema magufuli anawaachia wasiolipa kodi kwa kutowachukulia hatua na ndio watu haohao wanaolalamika kuwa Maghufuli ni dikteta kwa kuzihimiza mahakama kuhakikisha zinaharakisha taratibu za kisheria ili wahusika wote waliohusika na makosa ya kutolipa kodi wanachukuliwa hatua kutokana na makosa yao. Sasa hapo utaona watu wa upizani wamechanganyakiwa akiwemo mwanadiaspora wetu brother Libe. Kwa kweli mimi siwezi kuwalaumu watu wa upizani katika kuchanganyikiwa huko ule mziki wa Magufuli si mchezo hata waengereza wamemtaka David Cameron aige mfano wa Magufuli sasa hata wazungu wanamzimia sigara kuna chochote cha kubisha hapo juu ya uwezo wake? Na hizo siasa zao za majitaka za kujaribu kubeza ukweli wa hali halisi ya mafanikio makubwa ya kipindi kifupi ya Magufuli katika serikali yake ndicho kitu kitakachoumaliza upizani kwa sababu magufuli anapambana na hali halisi ya matatizo ya wananchi na wananchi wanaona laivu wakati wapizani bado wapo wamelala kulekule kwenye campaign na kutoa kauli, propaganda mgando zisizo na ukweli wowote na wananchi wanaelewa kuwa wapizani ni waongo kwani anachokifanya magufuli sio hadithi bali ni true story tofauti na ukiwasikiliza wapizani kwenye vyombo vya habari. Jambo jengine nachukua nafasi hii kumuonya brother Libe aachane kabisa na kauli za kibaguzi hizo za habari za kusema mpizani wake alikuwa mwarabu au bulushi huo ni upuuzi mtupu na ni dalili yakwamba brother Libe ameshindwa kisiasa na huo mpizani wake na sasa anajaribu kutumia race card hiyo ni hatari na sumu anayoitaka kuipandikiza kwa watu wake wa mbarali jambo ambalo ningemuomba brother Libe amsikilize mwalimu nyerere katika nasaha zake mwanzo kabisa wa hiki kipindi.