ANGALIA LIVE NEWS

Showing posts with label Jukwaa Langu. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa Langu. Show all posts

Monday, May 7, 2018

Kipindi cha JUKWAA LANGU, Mei 7, 2018

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo ndani ya Kilimanjaro Studios, wageni wetu studioni ni kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayoitumikia jamii ya wahitaji nchini Tanzania.
Katika saa la kwanza tutakuwa na uongozi wa SHINA INC ambao tangu mwaka 2002 wamekuwa wakisaidia jamii zenye uhitaji nchini Tanzania. Wana mengi ya kutushirikisha

Kwenye saa la pili tutakuwa na wakuu wa Help for Underserved Communities Inc. (HUC-USA) ambao wanajishughulisha kutoa textbooks mashuleni, VETA Scholarships na kusaidia matibabu ya macho nchini Tanzania.

Lakini tutaanza na mrejesho wa maadhimisho ya TANZANIA DAY 2018 yaliyofanyika Dallas Texas.

Ni kipindi cha JUKWAA LANGU, leo Jumatatu (Mei 7, 2018) na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Facebook live (Mubelwa Bandio na Kwanza Production) ama Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama piga simu 202-683-4570
*******************************
PRODUCER: Mubelwa Bandio

Wednesday, February 7, 2018

JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 2 TANO LADIES

Katika sehemu ya pili ya kipindi cha Jukwaa Langu Jumatatu hii tumetembelewa na TANO LADIES.
"Wadada" walioamua kuwa sehemu ya msukumo wa maendeleo ya wanawake na mabinti zetu.
Wamezungumzia (pamoja na mambo mengine) nafasi na mchango wao kama Diaspora kwa Tanzania, na pia wanavyopanga kuadhimisha siku ya kimataifa ya Wanawake duniani.
Unaweza ona sehemu ya video yao hapa
https://vimeo.com/253461804

JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi na waalikwa wengine kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf ama 202-683-4570
**********************************************
PANEL: Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe, Eddie Fundi

PRODUCER: Mubelwa Bandio

Kipindi cha JUKWAA LANGU Feb 5 2018 Pt 1 SARATANI

Katika sehemu ya kwanza ya kipindi cha Jukwaa Langu, tumezungumzia kuhusu siku ya SARATANI DUNIANI iliyoadhimishwa  Feb 4.
· Takwimu za maradhi haya zinaonyesha kwamba kifo 1 kati ya 6 hutokana na maradhi haya.
· Wajua, namna yanavyoathiri nchi zinazoendelea? Ni 20% tu zenye takwimu sahihi kuwezesha kupambana na maradhi haya.
Unajua ni tabia gani maishani zinaweza kuondoa 30% ya Saratani?
· Unafahamu harakati zinazofanywa na Diaspora katika kupambana na maradhi haya?
· Tulikuwa na Mwanasayansi na Mtafiti wa aina mojawapo ya Saratani, pamoja na mwanaharakati kujadili haya.
......
JUKWAA LANGU ni kipindi kinachoijadili TANZANIA YA SASA NA ILE TUITAKAYO. *Tanzania katika jicho la DIASPORA.*
Ungana na Mubelwa Bandio, Dj Luke Joe na waalikwa wengine studioni kujadili mambo mbalimbali kuhusu siasa, afya, uchumi, utamaduni nk.
Usikose.
Ni Jumatatu na kila Jumatatu kuanzia saa 12 kamili jioni mpaka 2 kamili usiku kwa saa za Marekani Mashariki (6:00 - 8:00pm ET)
Ni kupitia Kwanza Radio kwenye TuneIn
http://tun.in/sfwyf

Tuesday, September 27, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu Sep 26 2016...Wagombea uongozi DOCITA (Full)

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU cha Septemba 26, 2016 tulipata nafasi ya kuungana na wagombea wa nafasi za uongozi wa DICOTA kujadili mambo mbalimbali yanayoendana na uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba Mosi na Pili mwaka huu.
KARIBU

Monday, September 12, 2016

Kipindi Cha Jukwaa Langu Sep 12 2016....Tetemeko Bukoba

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU hii leo, tulizungumzia janga kuu la Tetemeko la ardhi nchini Tanzania
Wadau Baraka Galiatano wa BukobaWadau Blog na Erick Kimasha walijiunga nasi kwa njia ya Skype kutoka Tanzania kutupa taswira ya nini kilitokea, vipi kilipokelewa na maendeleo tangu Sept 10 na hali ilivyo hivi sasa mjini humo.
Pia tuliungana na mmoja wa wanaharakati ambao wameanzisha mfuko maalum kuchangia wahanga wa tetemeko hilo Agnetta .

Ungana nasi kuanzia saa 11 kamili jioni majira ya Marekani Mashariki (5:00pm ET) kupitia www.kwanzaproduction.com ama kupitia TuneIn tun.in/sfeLX
Kwa walio Marekani na Canada piga 240 454 0093
Karibuni

Tuesday, August 30, 2016

Kipindi cha JUKWAA LANGU Aug 29 2016 (Pt 1)...Demokrasia Tanzania

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA ya sasa na ile tuitakayo.
Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania na ukuaji wa Demokrasia ya nchi yetu.
KARIBU

Monday, August 29, 2016

Mahojiano na Prof Julius Nyang'oro katika kipindi cha JUKWAA LANGU

Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.
Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.
Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.
Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na mwanasheria
KARIBU
 

Monday, August 15, 2016

JUKWAA LANGU....Mahojiano na uongozi wa DICOTA unaomaliza muda wake

Katika kipindi cha JUKWAA LANGU cha Agosti 15, 2016 tulipata nafasi ya kuungana na uongozi wa DICOTA kujadili ulipo umoja huo wa waTanzania hapa Marekani na uchaguzi mkuu ujao
KARIBU

Mahojiano na Olympian Hilal Hemed Hilal (Live) kutoka Brazil

Photo Credits: MissiePopular.com
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU (Jumatatu Agosti 15 2016) Mubelwa Bandio alifanya mahojiano ya moja kwa moja na Hilal Hemed Hilal. Nahodha wa Tanzania katika mchezo wa kuogelea kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro nchini Brazil.
Alikuwa mkarimu kujiunga nasi kwa njia ya Skype sambamba na kocha wake Alexander Mwaipasi
Karibu uungane nasi

Monday, June 13, 2016

Jukwaa Langu Juni 13 2016....Msemaji wa serikali azungumza na Diaspora

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga
Photo Credits: Wavuti.com
Katika kipindi hiki, tumezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga ambaye ameeleza kuhusu nafasi na wajibu wa serikali kwa waTanzania waishio Diaspora.
Pia amegusia wajibu wa waTanzania hao kwa nchi yao na kujibu maswali mbalimbali
Karibu

Monday, June 6, 2016

Jukwaa Langu June 6 2016: Haki, Wajibu na Nafasi ya DIASPORA kwa Tanzania

Photo Credits: WikiProject African Diaspora
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tumejadili kuhusu DIASPORA.
Ni ipi nafasi, wajibu na haki yetu katika nchi yetu (Tanzania)?
Ni kweli kuwa tuna watu ama mahala muafaka kutuwakilisha nchini kwetu?
Na je! Tuna vyanzo halisi vya habari na taarifa kutoka Tanzania?
Tu,eumgama ma waTanzania wa Uingereza na Marekani kujadili hili

Tuesday, May 17, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu May 16 2016. Ziara ya Waziri mkuu UK. Uraia pacha

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London
Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA
Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.
Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.
Karibu

Monday, April 25, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu. Mjadala wa DICOTA Convention 2016 April 25

Kongamano la kila mwaka la waTanzania waishio Marekani (DICOTA) litafanyika mwishoni mwa juma hili jijini Dallas Texas.
Katika kipindi cha Jukwaa Langu jumatatu hii, tulipata fursa ya kuzungumza na viongozi waandamizi wa DICOTA, Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini Lunda Asmani na Mwenyekiti wa DICOTA Dr Ndaga Mwakabuta.
Pia wachangiaji mbalimbali
KARIBU

Monday, April 4, 2016

Jukwaa Langu (April 4) DICOTA Convention 2016

Katika kipindi hiki, tuliungana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa DICOTA Lunda Asmani na Mwenyekiti wa Jumuiya ya waTanzania jijini Dallas, Ben Kazora
Karibu

Monday, March 28, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu March 28 2016 (Full)


 Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA.
Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kujadili kuhusu Jumuiya za waTanzania nje ya nchi na changamoto zake, na pia kuhusu DICOTA na mkutano wao mkuu wa mwaka huu
KARIBU

Saturday, March 26, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu March 21 2016 (Full)

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA.
Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania
KARIBU

Tuesday, March 15, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu March 14 2016 (Full)

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu TANZANIA. Katika kipindi cha wiki hii, mbali na habari mbalimbali zilizotawala vyombo vya habari, pia wasikilizaji walipata nafasi ya kutoa maoni kulingana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania
KARIBU
Kipindi cha JUKWAA LANGU leo J3 kItaanza saa 11 jioni badala ya saa 12 ET
Kwa kusikiliza na kuchangia mada piga simu 240 454 0093 na ukipenda kuchangia boneza *5 pia unaweza kutupata kupitia tovuti zetu www.kwanzaproduction.com au www.vijimamboradio.com 

Pia ukipenda tunein tafuta Vijimambo radio

Tuesday, March 8, 2016

Kipindi cha JUKWAA LANGU na Mzee Emmanuel Muganda...(Mar 7, 2016)

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania yetu ya sasa na ile tuitakayo
Katika kipindi hiki utasikia mjadala tuliofanya na mtangazaji mkongwe Emmanue Muganda kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania
KARIBU

Thursday, February 25, 2016

Kipindi cha Jukwaa Langu Feb 22 2015. SIKU 100 ZA MAGUFULI

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Tanzania yetu ya sasa na ile tuitakayo

Katika kipindi hiki utasikia mjadala kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya 5 katika siku 100 za mwanzo

Tuesday, December 22, 2015

Kipindi cha Jukwaa Langu Dec 21 2015 (FULL)

Kipindi hiki hukujia kila jumatatu kuanzia saa 11 jioni kwa saa za Marekani ya Mashariki kuijadili Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Kuna mengi tuliyogusia pamoja na wasikilizaji wetu
KARIBU