Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu
amefanya Mabadiliko kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa na vikosi hapa nchini.
Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa kamanda wa
Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Leonard Paul amehamishwa
kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga
na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei
aliyekuwa Mkuu wa Utawala Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Mihayo Msikhela
aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga
amehamishwa kwenda kuwa Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia dawa za kulevya.
Aliyekuwa Kamanda
wa Polisi mkoa wa kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Ramadhani Mungi anaenda
kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Wilbrod
Mtafungwa ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Afisa
mnadhimu Mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Prudenciana Protas anakwenda
kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philipo Kalangi amehamishiwa Makao Makuu ya
Polisi na nafasi inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Shinyanga
ACP Ramadhan Ng’azi.
Aidha, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Camilius Wambura
anakwenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa Polisi ACP Francis Massawe kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dar es
Salaam.
Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP
Gilles Mroto anakwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya
kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Gemini Mushi aliyehamishiwa
Makao Makuu ya Upelelezi Dar es Salaam.
Wengine ni pamoja na Naibu Kamishna wa Polisi DCP
Hezron Gimbi anayetoka Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kwenda kuwa Mkuu wa Utawala Kanda
Maalumu Dar es Salaam pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Costantine Massawe
anakwenda kuwa Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.
Mabadiliko hayo ni ya kawaida kwa mujibu wa
Sheria, kanuni na taratibu za Jeshi la
Polisi.
Imetolewa
na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa
Jeshi la Polisi (T)
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment