Advertisements

Saturday, February 6, 2016

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM ZAENDELE HIVI SASA NDANI YA UWANJA WA NAMFUA MKOANI SINGIDA



 Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida.
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiwapungia mkono Wananchi waliofika kushuhudia maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM  mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, mkoani Singida.
 Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ukiwasili ndani ya uwanja wa Namfua mapema leo asubuhi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida
 Katibu Mku wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akimkaribisha Rais Dkt John Pombe Magufuli mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singid,pichani kati ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasilia mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua,mapema leo asubuhi ndani ya uwanja wa Namfua, kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM mkoani Singida.
 Baadhi ya Wananchi mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Namfua mkoani Singida hivi sasa. 

PICHA NA MICHUZI JR-MMG-SINGIDA

No comments: