Katibu
wa chama cha walimu manispaa ya Iringa mwalimu Fortunate Njalali akiwa ofisini kwake siku
kadhaa zimepita toka kufanyike uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la manispaa ya Iringa kwa ajiri ya kujadili baadhi ya agenda za kulijenga upya baraza
hilo, lakini chama cha walimu manispaa ya Iringa kimegoma kuhudhuria baraza hilo
kutokana na kukiuka baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali.
Akizungumza
na blog hii katibu wa chama cha walimu manispaa ya Iringa mwalimu Fortunate Njalali
amesema kuwa sababu ya kugoma kuingia kwenye baraza la halmashauri ya
manispaa ya Iringa kwa kuwa baraza hilo limepitwa na muda hivyo kunaitajika
kuliunda baraza jimpya ndio waweze kuingia kwenye baraza la wafanyakazi.
Aidha katibu
Njalali amesema kuwa wamekuwa wakiingia kwenye baraza la wafanyakazi kinyume
cha sheria kwa majadiliano maalumu hivyo walikuwa wakihudhuria baraza batili na
walikuwa wakimuambia mkurungezi juu ya swala hilo.
Njalali
amesema kuwa haiwezekani baraza la wafanyakazi likawa na viongozi wengi kuliko
wafanyakazi wenyewe hivyo watakuwa hawawatendei haki kwa kuwa hawatakuwa na
hoja za msingi zinazowahusu wafanyakazi wenyewe.
“Angalia
humu kwenye baraza hili tumejaa viongozi tu watumishe au walimu wenyewe
wanawakilishwa na nani na tutengemee matokeo gani kwa miaka ya baadae kwa
kupitisha bajeti isiyokuwa na mashiko kwa wahusika”.alisema Njalali
Njalali
ameongeza kuwa hawawezi kuingia kwenye baraza la wafanyakazi ambalo halina
viongozi kwa kuwa viongozi waliopo hawana uwezo wa kuwa viongozi wa kuongoza
baraza hilo kutokana na uwezo wao wa kitendaji.
“Hatuwezi
kuongozwa na wajumbe na viongozi haramu kwa kuwa wamekiuka sheria na
wanaijua hilo na kama mkurugenzi atandesha baraza hilo basi baraza hilo
litakuwa batili kwa kuwa chama cha walimu ndio waliosaini mkataba huo”.alisema
Njalali
Lakini
Njalalia ametangaza rasmi mgogoro na mkurungezi wa manispaa ya iringa kwa
kukiuka makubaliona waliokubaliana hapo awali wakati wa kusaini mkataba na
kuwahidi walimu kuwa watampeleka mkurugezi CMA
“Nimemwandikia
barua kuwa nimetangaza mgogoro na mkurugezi na nimempa siku tano kukutana na
viongozi wa chama cha walimu manispaa ya iringa vinginevyo tarehe kumi na sita
mwezi huu nampeleka kwenye baraza la usuruhishi CMA kwa kukiuka sheria na
makubailiona ya mkataba wetu”.alisema Njalali
Njalali
alimalizia kwa kusema kuwa baraza la wafanyakazi linafaida kwa watumishi kwa
kuwa wanajadiliana na muaji wao juu ya mazingira ya kazi yao na wafanya nini
ili kuboresha ufanyaji wa kazi zao na kuongeza ubunifu wa kuboresha kazi.
“Tumekuwa
tunapitisha bajeti nyingi lakini hakuna mrejesho wowote ule wa ile bajeti
tunayoipitisha hivyo tumekuwa tunaburuzwa mara kwa mara kwa sasa basi
hatutaki kuburuzwa tena tunataka haki yetu na ndio maana tumetangaza mgogoro na
mkurugenzi wa manispaa ya Iringa”alisema Njalali.
Tulipomtafuta
mkurugezi wa manispaa ya iringa hakupatika kujibia kero hii iliyotolewa na
katibu wa CWT,hata hivyo baraza la wafanyakazi lilifanyika na wakafanya
uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya wa baraza hilo.
No comments:
Post a Comment