ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, February 18, 2016

TASWIRA TANO ZA CHIMBO LA YANGA HUKO KISIWANI PEMBA


Yanga inajiandaa kuivaa Simba keshokutwa Jumamosi. Imeamua kwenda kujichimbia kisiwani Pemba.
Kisiwani humo Yanga inaishi katika Hoteli ya Misali Beach Resort ambayo ni bora hasa katika mji wa Pemba.
Iko katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, ikiwa na mazingira tulivu huku vyumba vyake vikiwa vimejengwa kwa mfumo wa vibanda unaotoa nafasi ya wapangaji wake kujipumzisha kwa nafasi.
Mara kadhaa, Yanga imekuwa ikiweka kambi katika hoteli hiyo na mara ya mwisho ni mwishoni mwa mwaka jana ilipoweka kambi, iliporejea kurejea Dar es Salaam ikapata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba.

No comments: