Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam leo wakati alipozungumzia mpango wa kuwasafirishwa walimu bure jijini Dar es salaam wakati wa kwenda na kurudi kazini huku akiwa ameongozana na viongozi wa vyama vya usafirishaji wa abiria jijini Dar es salaam pamoja na viongozi wa Madereva wa Daladala jijini Dar es salaam.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog)
Mwenyekiti wa Chama Chama Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es salaam, Said Mabrouk(wa kwanza kushoto) akizungumzia mwitikio wa wamiliki hao kuhusu kuwasafirisha walimu ili kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Konondoni Mh. Paul makonda na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kutoa elimu bure hapa nchini, kutoka kulia ni Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Madereva, Shabani Mdemu, wa pili kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wasafirishaji abiria Dar es Salaam, (UWADAR),William Masanja akizungumza na waandishi wa habari leo jijinni Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini
Na Chalila
Kibuda, Globu ya Jamii
WALIMU wa
Shule ya Msingi na Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam watasafiri na Daladala bure
kuanzia Machi 7 mwaka huu.
Akizungumza
na waadishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda amesema kuwa kutokana na changamoto za walimu ameona kuna umuhimu wao
kusafiri bure waweze kupunguza makali ya nauli za kila siku wanapopanda
daladala hizo.
Amesema kuwa
walimu watasafiri kwa kwa usafiri huo kuanzia saa 11:30 hadi saa 2 kwa muda wa
asubuhi na baada ya muda huo kupita watalipa nauli zao na nyakati za jioni
watarudi majumbani mwao kwa kupanda daladala hizo kuanzia saa 9 hadi saa 12.
Makonda
amesema kuanzia kesho watatengeneza vitambulisho vya walimu wote wa serikali wa
mkoa wa Dar es Salaam ambavyo wataonyesha kwa makondakta wa daladala vikiwa na
saini ya mkuu mkuu wa Wilaya.
Amesema
utaratibu huo utakuwa ukitumika kwa siku za kazi tu kwa walimu kupanda bure na
sio vinginevyo na walimu wanaoishi mikoa mwingine na wanafundisha Dar es Salaam
watalipa nauli zao kufika katika vituo vyao vya kazi.
Aidha
amesema kuwa walimu wataingia katika Daladala wasiopungua wawili na wengine
watasubiri daladala zingingine kutokana na maoni ya wamliki wa vyombo vya
usafiri.
Nae
Mwenyekiti wa Umoja wa Wamiliki wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam, Sabri
Mabroock amesema kuwa wanaunga mkono sera ya elimu ya Rais Dk.John
Pombe Magufuli.
Amesema
walimu wamekuwa na changamoto wakati mwingine wanashindwa kulipa hata nauli
hivyo kupanda bure watakuwa wamerahisisha maisha.
No comments:
Post a Comment