ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 17, 2016

WAZIRI KITWANGA AKABIDHIWA RIPOTI YA MPANGO WA UTEKELEZAJI WA KUBORESHA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kushoto) akipokea ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akisaini ripoti aliyokabidhiwa na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia), kwa ajili ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa Jeshi la Polisi. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi hivi karibuni kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kumkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Issa alisema Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni. Hafla hiyo fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (wapili kulia) akzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) na Maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi la Polisi. Katika hotuba yake, aliwataka Polisi wahakikishe wanautekeleza Mpango huo na kila wiki ameagiza apewe ripoti ya utekelezaji huo unaotarajiwa kuanza katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Kulia ni Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa. Wapili kushoto meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu. Kushoto meza kuu ni Naibu IGP, Abdulharam Kaniki. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Christopher Fuime.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati), ripoti ya Mpango wa Utekelezaji wa Kuboresha Usalama wa Raia na Mali zao kwa ajili ya Jeshi lake. Waziri Kitwanga alikabidhiwa ripoti hiyo na Mtendaji Mkuu Ofisi ya Rais ya Kuratibu Utekelezaji wa Miradi (PDB), Omary Issa (kulia) katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Mpango huo unatarajiwa kuanza rasmi kwa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni na baada ya hapo utasambaa nchi nzima. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

2 comments:

Anonymous said...

Kwanini kila kitu lazima kianze Dar eS Salaam? Ndiyo maana watu wanakimbizana kujazana huko Dar. Kwanini usianze mikoa mingine? BTW huo mpango unasemaje? Tunataka tuelezwe maana kuna mambo mengi hayakai sawa kama utoaji wa PF 3 huo ni janga la taifa, badala ya kuwahisha wagonjwa hospitali wenye emergency unaenda kwanza polisi na mara nyingi wako polepole sana au hayupo mhusika.....sasa mgonjwa/majeruhi atapona hapo, nyingine kikubwa ni kuwa polisi wetu hawatumii sharia bali utashi wao, utawakuta wao ndiyo mahakimu wa kutoa maamuzi yote bila kujali kuwa wanawaonea wengine, mapolisi wengi wanafuta kesi kwa utashi wao. HAYA YOTE YANAFAA YAWEPO KWENYE HIYO RIPOTI VINGINEVYO MNAPOTEZA MUDA.

Anonymous said...

Mdau hapo juu, kwanini daresalam?
Daresalam kwa Tanzania ni sawa na kichwa katika mwili wa mwanadamu anapoanza kuoga au kuusafisha kwa kuanzia kujimwagia maji kichwani kuna asilimia kubwa mwili wote kupata maji haraka kuliko ukianzia miguuni.