Baada ya rapa Chidi Benz kuomba msaada ili asaidiwe kuirudisha afya yake ambayo imethorofika kutokana na matumizi ya Madawa ya kulevyana na baadae kusaidiwa na Babu Tale kwa kupelekwa rehab. Wadau mbalimbali pamoja na wasanii wenzake walimpongeza Babutale lakini Dudu Baya amedai hakupenda rapa huyo asaidiwe.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Dudu amedai rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa ndio maana baada ya kusaidiwa anataka kujipangia baadhi ya mambo.
“Watu mfano wa Chidi Benz hawatakiwi kusaidiwa, niwakuachwa wafe na wazikwe. Kwanza ni waongo, ukikutana nao utasikia naumwa au nimefiwa, utampa msaada, mwisho wa siku anaenda kujidunga. Misaada kama hii inatufanya majina yetu kuwekwa kataka orodha ya wauaji (killers),” alisema Dudu.
Aliongeza, “Babutale na wenzake walipomfisha Chidi Benz rehab kwanza alianza kuweka masharti yake kituoni, mara hawezi kushauriwa na mtu ambaye hajawahi kutumia sumu hiyo (unga). Hapo ndipo nilipogundua amebebwa kinguvu bila yeye kuwa tayari kupona. Ni sawa na mgonjwa apelekwe hospitali then aanze kutoa masharti yake, eti hiki kitanda sikitaki. Wewe dokta huwezi kunitibu kwa sababu hujawahi kuumwa ugonjwa ninaoumwa, mgonjwa kama huyo si nachotaka ni kifo?. Hata wakati yesu amekuja kutukomboa na dhambi, aliponya wagonjwa waliokuwa tayari kupona, hata leo umpeleke ndugu yako kanisani au msikitini akaombewe aache ulevi au umalaya, kama hana dhamira ndani ya moyo wake ya kuacha, hakiwezi tokea chochote,”
Pia Dudu amesema wasanii wengi wanasikia kila siku kuhusu madhara ya Madawa ya kulevya lakini wanapuuzia.
“Chidi Benz si mtoto mdogo, ameshuhudia wasanii na watu wa kawaida wengi tukiwapoteza kwa sababu ya Madawa ya kulevya lakini wanapuumzia, wanarudia kubwia tena. iweje leo yeye ajiingize kataka ulimwengu huo? hakika kifo anakitaka mwenyewe na si kurubuniwa. Uzuri wa Tanzania hatuna umasikini wa ardhi, watu kama hawa hawana faida kwa taifa, niwakuacha wafe na wazikwe. Na kama inawezekana Mh Rais Magufuli angetoa amri mateja wakifa wazikwe na jiji. Kwa sababu sioni ndugu yeyote wa Chidi yuko bize na rapper huyo. Kwanini nyingi mumpaparikie au ndio mnauchukungu kuliko ndugu zake?. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu,” alisema Dudu. Nini mawazo yako juu ya maneno ya Dudu Baya!!???.
Bongo5
2 comments:
Amesema vizuri tena angeshindiria msumari haswaaa. Kwani ushamba wa pesa unawasumbua vijana wetu.
Vijana lazima wajue ,kwanza unga hauonjwi , pili muuzaji mwenyewe hatumii tatu ulijaribu kutumia hata kwa kujificha , mwisha wake ni Uchid Benz au RC tu hakuna mwisho mbadala wa mtumia unga zaidi ya kuadhirika ! Unga usisubutu kutumia wala Usijalibu ! tahadhali kwa mwenye akili tu Unga hauonji !
Post a Comment