Wawakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB) wakifuatilia mkutano uliofanyika katika makao makuu
ya Wizara ya Nishati na Madini ambao ulijumuisha watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini na
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kutoka kulia Kulia ni Lucio Monari, Natalia Kulichenko,
Vladislav Vucetic na Emmanuel Mungunasi.
Watendaji kutoka Benki ya Dunia (WB) wamefika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini ili kuzungumza na wataalam wa Wizara na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati nchini.

Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile (wa pili kushoto),
akiwasikiliza Watendaji wa Benki ya Dunia waliofika katika Wizara ya Nishati na Madini ili kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Nishati nchini. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi
wa Nishati anayeshughulikia Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma na Wa Pili kulia ni Kaimu Kamishna
Msaidizi wa Nishati anyeshughulikia Gesi Asilia, Ebahart Diliwa.
Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli , James Andilile (mwenye suti ya kijivu),
akizungumza jambo katika mkutano baina ya Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, TANESCO,
na watendaji kutoka Benki ya Dunia (WB).
No comments:
Post a Comment