Thursday, March 3, 2016

Makamu wa Rais. Mhe. Samia Suluhu Hassan afungua Mkutano wa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wabunge waliohudhuria Mkutano wa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki baada ya kufungua Semina ya siku mbili (EALA) leo Jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akiwahutubia Wabunge waliohudhuria Mkutano wa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki (EALA) leo Jijini Dar es Salaam.

Baadhi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Mkutano wa Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki (EALA) leo Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye ushungi) akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo baada ya kufungua rasmi Semina ya siku mbili inayofanyika jijini Dar es Salaam.

(Picha zote na Benedict Liwenga)

No comments: