ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 1, 2016

NAY WA MITEGO:SITO RUDI NYUMA KUWAAMBIA UKWELI WATU WANAOFANYA MAMBO YASIYO NA TIJA.


Licha ya kukumbwa na misukosuko ikiwamo kuvunjiwa kioo cha gari yake,Rapa Nay wa Mitego amesema hatarudi nyuma kuwaambia ukweli watu wanaofanya mambo yasiyo ya tija.

Wiki iliyopita msanii huyo alivunjiwa kioo cha gari lake na watu wasiojulikana wakati akienda kutambulisha video ya wimbo wake mpya wa ‘Shika Adabu Yako’ kwenye kipindi cha televisheni.

kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii raoa huyo,Nay ameweka picha ya gari hiyo ikiwa imevunjwa juii huku akiwaomba radhi mashabiki wake kwa kushindwa kuweka video hiyo kwa muda mwafaka kutokana na tatizo hilo.

”Mimi ninafarajika sana kwa sababu kile ambacho nimekikusudia kukifikisha kwa walengwa,kimefika na ninawaomba mashabiki wangu waendelee kuniunga mkono katika harakati hizi za kuelimisha watu kuachanana mambo yasiyofaa,”alisema Nay

No comments: