ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 13, 2016

TANZANIA NA UENYEKITI WA KUNDI LA NCHI ZA AFRIKA KATIKA UMOJA WA MATAIFA

Balozi Tuvako Manongi akimkabidhi zawadi ya kumuanga kwa niaba ya Mabalozi wenzie aliyekuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Liberia katika Umoja wa Mataifa, Balozi Marjon V. Kamara ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Liberia.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dr. Albina Chuwa akitoaa raarifa fupi kwa niaba ya Wakurungezi Wakuu wa Idara za Takwimu kutoka Nchi za Afrika kuhusu maazimio na mapendekezo yao kuhusu viashiria vya ajenda ya Maendeleo Endelevu. Kulia kwa Balozi Tuvako Manongi ambaye Tanzania ni Mwenyekiti wa Mwezi wa nchi za Kundi la Afrika ( African Group) Ni Mtakwimu Mkuu kutoka Ivory Coast
baaadhi ya Mabalozi na Maafisa
baaadhi ya Mabalozi na Maafisa
Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi wa Idara ya Siasa ya Umoja wa Mataifa, Bw. Taye-Brook Zerihoun naye akiwasilisha taarifa yake kwa Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba wawakilishi hao kuunga mkono pendekezo la Idara yake la kupatiwa fedha ambazo wanataka kuzitumia katika eneo la uratibu na usimamia wa majadiliano kuhudu dhana nzima ya uzuiaji wa machafuko ( mediation and prevention ) pamoja na kuongeza ajira.
Mkurugenzi Mkuu wa UN-Women Phumzile Mlabo Ngcuka akiwaeleza Mabalozi kuhusu mkutano wa 68 wa Kamishini Juu ya Hali ya Wanawake utakaoza siku ya Jumatatu hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,Mada kuu ya Mkutano wa mwaka huu ambao huwakusanya mamia ya viongozi wanawake kutoka mataifa yote duniani ni Uwezezaji wa Wanawake kupitia utekelezaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu ( aganda 2030) Kushoto wa Balozi Manongi ni Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika Umoja wa Mataita, Balozi Antonio Tete
Sehemu ya Mabalozi na Maafisa kutoka nchi Wanachamawa Umoja wa Afrika wakifuatilia mkutano.


Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, kupitia  Uwakilishi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa,   ni Mwenyekiti wa Kundi la  Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa March. Miongoni mwa majukumu ya  Mwenyekiti wa Mwenzi ni pamoja na  kuitisha , kuratibu na kuendesha mikutano   inayowahusisha  Wawakilishi wa Kudumu  kutoka Nchi 53 wanaoziwakilisha  Nchi zao katika Umoja wa Mataifa.
Mwenyekiti wa  mwezi,  pamoja na  kuratibu na kuendesha mikutano  yenye ajenda mbalimbali pia anawajibika katika  kuwasilisha kauli ya  nchi za Afrika kupitia ama utoaji wa hotuba au  mawasiliano na Wakuu  wa Idara mbalimbali ndani ya Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa, akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pale  inapolazimu.

Pichani ni baadhi ya Matukio yaliyotokea mwishoni wa wiki wakati wa Mkutano  wa  Wawakilishi hao wa Nchi za Afrika  chini ya  uenyekiti wa Tanzania,  ambapo  walipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa watendaji wa Umoja  wa Mataifa pamoja na  taarifa kutoka kwa Muungano wa Wakuu wa  Idara za Takwimu kutoka  Afrika waliokuwa wakishiriki katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.   

No comments: