ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 27, 2016

TASWIRA YA KWENYE KISOMO CHA BABA YAKE MKUBWA MWENYEKITI WA CCM-NY (Seif Akida)


Sheikh Bashir kutoka Connecticut akiongoza Dua kwenye 
kisomo cha marehemu mpendwa baba yao mkubwa Akida, na Salimu wa New York kisomo hicho kilifanyika Jumamosi ya tarehe /26/3/2016), 2505 Third avenue, Bronx, NY na kuhudhuliwa na marafiki kutoka Boston, Connecticut na New Jersey.


Bwana Seif Akida (mfiwa) akisikiliza dua ya kumuombea baba yake mkubwa na kushoto kwake ni mzee Lucas rafiki mkubwa wa Bwana Seif.


Sheikh Bashir katikati na kulia ustadh Al Hajj Kibodya kutoka Springfield na kushoto ni Dr Abbas .Kwa taswira zaidi unaweza kwenda kwa kubonyeza soma zaidi. 


6 comments:

Anonymous said...

inna lillahi waina illahim rajiun.poleni sana family yote ya seif akida.Allah akupeni moyo wa kustahamili.na inapendeza sana kuona waislamu mnashikana huko marekani na ulaya pamoja na ndugu zetu wasio waislamu kukuungeni mkono na kuwa kitu kimoja. Utanzania wetu ndo hazina yetu.Allah akujaliyeni kila la kheir na kizazi chenu mshikamane daima kwenye dhiki na furaha muondoe tafauti zenu muwe kitu kimoja popote pale mlipo.amin.

vijimambo team wote shukran kwa picha hizi.Allah akulipeni kila la kheir.amin

Anicetus said...


Annoymous march 27, 2016 at 6:30 amesema: "Utanzania wetu ndo hazina yetu". Ni maneno yenye busara sana na sisi watanzania wa ugaibuni tuko pamaoja wakati wa kilio na furaha. Hatuoni kabila,rangi, dini,cheo, tajiri nakadhalika. Uongozi wetu ni mfano wa kuiga.

Anonymous said...

MAMBO MATATU AMBAYO YATAKAYOMFAA MAITI NI
1. SWADAQA YENYE KUENDELEA (KISIMA, SEHEMU YA MASOMO, SEHEMU YA MATIBABU, SHAMBA N.K )
2. ELIMU YENYE MANUFAA ( ALIYESOMESHWA NAE AKASOMESHA IKAENDELEA TUU ELIMU HIYO )
3. MTOTO MWEMA ( ATAKAEKAA NA KUMUOMBEA DUA MZEE WAKE , MUNGU AMUONDELEE ADHABU ZA KABURI)

KUKUSANYIKA WATU WAKASEMA WANAMUOMBEA DUA ALIEKUFA HUO NI UZUSHI ULIOZUSHWA BAADA YA MTUME MUHAMMAD SWALA LLAAHU ALAYHI WASSALAM KUFA, NA KARNE KUPITA.
KUTOKANA NA HADITHI YA MTUME KILA KIZUSHWACHO NI BIDAA NA KILA BIDAA NI MOTONI.
WANAPOSEMA WATU KUNA UBAYA GANI SI NI KISOMO?
UBAYA UPOO KWA SABABU MTUME ALITUMWA KUJA KUONGOZA NA KABLA YA KUFA KATIKA HIJJATU WADAA ALIWAHUTUBIA WAISLAM NA KUWAAMBIA KUWA AMEKAMILISHA DINI, SURATIL MAAIDAH AYA YA TATU,MWENYE KUTAKA KUSOMA ZAIDI ATAONA.
KWA HIVYO DINI HAITAKIWI KUPUNGUZWA AU KUONGEZWA, KILA KITU KIMESHAKAMILISHWA NA MTUME MWENYEWE. TUSIWE WENYE KUONGEZAONGEZA,
KUFANYA HIVYO INA MAANA MTUME HAJAKAMILISHA DINI SASA WATU NDIO WAMEKUJA KUIKAMILISHA.
OGOPENI MOTO, MOTO AMBAO KUNI ZAKE NI WATU.
WANAPOSEMA WATU HAYA MAMBO YAPO ZAMANI MBONA,TOKA ENZI ZA MABABU NA MABABU HITMA, MAULIDI N.K
ENHE,WALIPOKUWA WANAONYWA QAUMU ZILIZOPITA, WATU WA ADI, THAMUDU, LUUT, IBRAAHIM,HUUD, WALIKUWA WAKISEMA KUWA HAYA MAMBO TUMEWAKUTA NAYO BABU ZETU NA VIZAZI VILIVYOPITA KWA HIVYO HATUWEZI KUYAWACHA HAYA, (INGIA KWENYE QURAN UTAKUWA YOTE HAYA NISEMAYO)
SASA NDIO SISI TUNAPOKATAZWA JAMBO TUSIFANYE, TUNAKUWA NA MIDOMO MIREFU KUJIBU BILA YA KUWA NA REFERENCE.
MUHIMU NI KUTAFUTA ELIMU SWAHIHI NA KUTAFAKARI KWA KILE UNACHOKITAFUTA NA KUKIFANYIA KAZI.
NAWEZA KUKUPA MFANO HAI, HAPO WATU WAMEKUSANYIKA KWA AJILI YA KISOMO, HIVI KWELI HAPO WOTE WALIOKUJA WAMEKUJA KUSOMA AU KILA MTU KAJIA LAKE.
NISAIDIE KIDOGO KULA AMBAO WALOKWENDA KWA AJILI YA MLO, KUNA AMBAO WALIOKWENDA KWA AJILI YA KUONANA TUU NA WENZAO HAWAJAONANA SIKU NYINGI, KUNA WENGINE KWA AJILI YA MWENZAKE KAMWAMBIA NA YEYE KAFATA TUU, UNAWEZA KUWAPATA WALIOKWENDA KIDHATI KWA AJILI YA KISOMO NI WACHACHE KWELI , NA HATA HIVYO KISOMO HICHO NI CHA BIDAA , BUREEE , WASITARAJIE KUWA NDIO MAITI KIMEMFIKIA, HAMNA.
MAITI HUNUFAIKA NA HAYO MAMBO MATATU YALIOPO HAPO JUU.
KUHUSU MSHIKAMANO WA WATU NI VIZURI KUSHIKAMANA ILA MISHIKAMANO ISIWE KWA AJILI YA MILOO, IWE MISHIKAMANO KWA AJILI YA MWENYEZI MUNGU.
MFANO.
KUNA MGONJWA, VIZURI WATU WAKASHIKAMANA KUFANYA UTARATIBU WA KWENDA KUMUANGALIA NA KUMSAIDIA KIMAWAZO, KIFEDHA N.K.
KUNA MTU AMEFILIWA, KUMPA MCHANGO WA KUMSAIDIA NA KILA MTU AENDE KWA WAKATI WAKE, KUMPELEKEA CHAKULA, SIO TENA NA WEWE UNAKAA HAPO HAPO UNAKULA.
NA MSIBA NI SIKU TATU TUU, IKIMALIZA SIKU TATU HAMNA TENA MSIBA. WALA MIKUSANYIKO HAYO NI MAMBO YA KIZUSHI.
NA MENGI MENGINAYO
NAHOFIA KUWACHOSHA WASOMAJI LKN NATAMANI NIENDELEE KUANDIKA TUU.

UKIONA NILICHOKIANDIKA KIMEKUPATA, UJUE KUWA HIYO NDIO DAWAA, VUMILIA IMEZE NA REJEA KUITUMIA TENA MPAKA IKUTIBU.
UKIONA NILICHOKIANDIKA NI UPUUZI, UJUE KUWA WEWE NI MTOTO WA IBILISI NA YAMEKUKASIRISHA YALIOANDIKWA KWA SABABU UNAONA HUTOWAPATA WENGI KUINGIA NAO MOTONI.
UKIONA NILIOANDIKA NI YA MAANA, UJUE YA KUWA AKILI YAKO IMEFUNGUKA NA UMEWEZA KUTAMBUA HAKI NA BATILI NA MWENYEZI MUNGU AKUHIFADHI UZIDI KUTAFUTA ELIMU.
KWA WALE AMBAO WATAKAOSOMA AMBAO SIO WAISLAM, WAJUE TUU YA KUWA HUU NI UKUMBUSHO WA WAISLAM,NI WAJIBU WA BINAAAMU KUKUMBUSHA MARA KWA MARA KUTOKANA NA TABIA ZETU ZA KUGHAFILIKA. KWA HIVYO WANAWEZA KUFAIDIKA NA UKUMBUSHO HUU AU WANAWEZA WAKAUACHIA KAMA ULIVYO.

Anonymous said...

Annony wa Mambo Matatu si ungejitambulisha basi? Uannonymous wa nini kama wewe umeielewa sana maana ya Ibada na Swala hiyo?

Anonymous said...

jamani kushika quran bila ya udhu na mhusika akiwa si muislamu inakuwaje?
naomba nielimishwa.shukran.

Anonymous said...

mdau wa 6:58 umesema kweli ila kama watu wanamrehemu mzee wao wache tu wafanye hivyo huwezi kujua faraja yao rohoni ikoje wakiwa wanafanya jambo hilo.

lakini ki haki hakika umesema ukweli mtupu na mambo yote tunayaona tunapokushanyika huku.