ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 25, 2016

WAHOLANZI WAWILI WAKAMATWA UWANJA WA NDEGE WA KIA NA TUMBILI 61

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa akiwa ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuzungumza na wanahabari.

 Na Dixon Busagaga.

VYOMBO vya ulinzi na usalama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) vimefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wawili ndugu ,raia wa Uholanzi wakiwa katika harakati ya kusafirisha wanyama Hai 61,aina ya Tumbili kuelekea nchini  Armenia.


Wanyama hao wakiwa kwenye makasha sita tofauti ya kuhifadhia wanyama walikuwa wasafirishwe kwa ndege maalumu ya mizigo yenye namba EW/364G iliyosajiliwa nchini Belarus kupitia kampuni ya Arusha Freight Limited ya jijini Arusha.


Raia hao wa Uholanzi waliokamatwa juzi majira ya saa 1:30 jioni katika uwanja wa ndege wa KIA wametambulika majina yao kuwa ni Arten Vardanian (52) aliyekuwa na hati ya kusafiria yenye namba NWF8CKJR8  na Edward Vardanian (46) aliyekuwa na hati ya kusafiria namba NY969P96.

Meneja usalama uwanja wa ndege KIA,Kisusi Justine aliliambia Tanzania Daima mbali na kukamatwa kwa raia hao wa kigeni pia walifanikiwa kumshikilia Mtanzania ,Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.


“Wahusika hawa wawili walifika eneo la Cargo ambako walikuwa katika harakati za kusafirisha wanyama hao ndipo tulipowashikilia kwa sababu taratibu za kusafirisha wanyama Hai zilikiukwa”alisema Justine.


Kuhusu mazingira ya kukamtwa kwa watuhumiwa hao ,Justine alisema ndege hiyo inaonekana ilitua katika uwanja huo mahususi kwa ajili ya kubebeba wanyama hao na kwamba ili ruhusiwa kuondoka jioni ile baada ya kukamatwa kwao.


Kamnda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna msaidizi wa Polisi ,Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kukamatwa kwa raia hao na kwamba wamehifadhiwa katika kituo cha Polisi cha KIA huku uchunguzi zaidi ya tukio hilo ukiendelea.


“Mnamo Machi 23 mwaka huu majira ya saa 1:30 jioni huko uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA ) tulifanikiwa kuwakamata raia wawili wa Uholanzi wakiwa wanataka kusafirisha wanyama aina ya tumbili na tayari uchunguzi kwa kushirikiana na Wizara ya maliasili na Utalii unaendelea”alisema Mutafungwa.


Kamanda Mutafungwa alisema taarifa za awali zinasema wanyama hao waalisafirishwa hadi uwanjani hapo wakitokea mpakani mwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo kampuni ya uwakala ya Arusha Fright Limited ilipewa kazi hiyo.


Alisema uchunguzi wa awali unaonesha ndege ya mizigo iliyokuwa isafirishe wanyama hao ni ya binafsi huku akikanusha kukamatwa kwa mtu mwingine anyetajwa kuhusika katika kuuza wanyama hao kwa raia hao wa Uholanzi.


“Mpaka sasa tumewakamata hao raia wawili ,lakini kama nilivyosema uchunguzi unaendelea tukishirikiana na wizara ya maliasili na utalii ili tuone kama kuna washiriki wengine wa tukio hilo ,so far tunao hao wawili tu”alisema Mutafungwa.


Alisema mbali na hati za  raia hao wa uholanzi kuonesha kuwa walikuwa wakiishi nchi kihalali bado vyomb vya ulinzi na usalama ikiwemo idara ya Uhamiaji vimeanza kuchunguza pia uhalali wa vibali vya raia hao vya kuishi nchini.

1 comment:

Anonymous said...

Hivyo ndivyo rasilimali zetu zinavyotoroshwa kiholela na siku zote tunasema mvunja nchi ni wananchi mwenyewe. Na hao waholanzi wanaodaiwa kuishi kihalali huku wakijishughulisha na vitendo haramu vya kuziangamiza rasilimali za nchi yetu kwa kweli wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na wale wote waliohusika. Ikiwezekana kufungwa jela na wakishatumikia adhabu yao jela wasiruhusiwe kuishi tena nchini. Kwa sababu inawezekana kabisa kuwa hiyo sio mara yao ya kwanza katika kujihusisha na vitendo kama hivyo. Na inawzekana kabisa hao tumbili sio mzigo wenyewe hasa kwa kawaida ya wafanya biashara ya magendo wanapojaribu kuanza kupitisha biashara zao haramu aidha katika kituo kipya au sehemu yenye mabadiliko ya uongozi au hata kumjaribu msafirishaji mpya mara nyingi huwa wanatuma mzigo wenye thamani ndogo kuangalia hali halisi ikoje. Kwa hivyo tunaweza kusema walikuwa wakimjaribu Magufuli na serikali yake ipo vipi? Kwa kifupi tungeiomba serikali ya Magufuli kupitia tena upya mikataba yote ya wale tunaowaita waekezaji wakigeni na hata wazawa waliowekeza katika rasilimali zetu kama migodi ya madini na wale wenye kumiliki vitalu vya uwindaji katika mbuga zetu nakadhalika. Katika hali ya kawaida mtu wala haitaji utafiti yakwamba serikali ya awamu iliyopita ilikuwa haipo fit kuingia mikataba na muekezaji yeyote yule kutokana na watumishi wake wengi kuwa corrupted. Angalia mifano kidogo tu,watumushi hewa kila sehemu,Mikataba hovyo ya uzalishaji umeme, utoroshwaji uliokisiri wa mapato ya serikali nakadhalika nakadhalika. Sasa leo watu hao unieambie unaweza kunifanya niamini yakuwa watakuwa wasafi katika kufunga mikataba ya tanzanite? Dhahabu? Almasi na Gas? hata siku moja na ndio maana kenya na India zinajulikana kama the world number one tanzanite producer. Tanzania ina Dhahabu na Almasi za kiwango cha kuleta ushindani duniani kama kungelikuwa na usimamizi mzuri lakini zote zinaishia kw wajanja na kama utamwambia mtu huku nje kwamba Tanzania tunadhahabu na Almasi anakushangaa. Hata zile sehemu au maeneo yanapotoka hayo madini wakazi wake bado ni wanyonge wakati hao wachache wageni wanaomiliki hiyo biashara ya madini kama utapeleka spy kuwafuatilia utajiri wao unaweza hata usiamini unachokiona. Watanzania wakati wa kulala umepita inabidi tuamke la sivyo licha ya nchi yetu kuwa na rasilimali za kutosha lakini tusipokuwa makini tutaishia patupu na mbaya zaidi ni ile hali yakuwa watumwa ndani ya nchi yetu tukitumikishwa kinyonge kutokana na rasilimali zetu wenyewe.