Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
BAADHI ya wazazi wa wanafaunzi
waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa
Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha
matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.
February 26 mwaka
huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo kikuu cha St Joseph
(SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita tangu kuchukuliwa kwa hatua
kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea,vyuo vilivyoko chini ya
shirika la kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI).
Wakizungumza na
mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku
wakidai kuwaathili kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika
maandalizi ya mitihani.
“Nadhani ingekuwa ni
jambo la busara kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na uongozi wa chuo
badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki kimekuwa kikitoa
mchango mkubwa katika kuzalisha wataalumu mbali mbali.”alisema Mrisho Sume.
Nchi yetu ina
wataalamu wachache katika sekta ya
Sayansi na Teknalojia ,chuo hiki kilikuwa ni kimojawapo kinachotoa wataalamu
hao hivyo mchango wake unapaswa kuheshimika na kusaidiwa pale inapobidi,” aliongeza
Sume ambaye mwanaye alikuwa akisoma katika chuo cha Sayansi ya kilimo katika
chuo hicho tawi la Songea.
Mzazi mwingine
alijitambulisha kama Mariam Ali alisema taarifa alizokuwa nazo ni kuwa uamuzi
wa kufunga baadhi ya matawi hayo ulifikiwa bila ya kukipa taarifa chuo hicho
juu ya mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kukipa muda wa kuyafanyia kazi.
“Binti yangu alikuwa
akisoma tawi la Arusha na nimepata taarifa kuwa timu ya ukaguzi kutoka
tume ilifika chuoni hapo kwa ajili ya ukaguzi lakini cha kushangaza
ni kuwa chuo hakikupewa taarifa ya mapungufu yaliyoonekana ili yafanyiwe kazi
na badala yake kililetewa barua za kufutiwa vibali.”alisema Mariam.
Uamuzi ulifanywa ni
wazi haukuzingatia haki na unatuumiza sisi wazazi pamoja na watoto wetu,
tulitegemea TCU kukipatia chuo ripoti ya mapungufu waliyoyagundua na
kupewa muda wa kuyafanyia kazi na endapo kingeshindwa kuyafanyia kazi
katika muda ambao kimepewa tume ingekuwa na haki ya kutoa adhabu,” aliongeza
Mariam.
Naye John Budigle
alisema tangazo lilitolewa na TCU kuhusu kufunga vyuo hivyo lilisema moja ya
matatizo yaliyopelekea kufungwa ni migomo ya wanafunzi huku akiongeza kuwa migomo
yote ilitokana na kucheleweshewa mikopo
na siyo matatizo ya chuo .
“Mimi kwa mtizamo
wangu naona kama TCU imetumia nguvu kubwa kwenye suala hili, kama chuo
kilifanya makosa kilipaswa kupewa maelekezo ya kushughulukia kasoro au
mapungufu kwani hakuna chuo kisichokuwa na mapungufu hata hivyo vya umma. “alisema
Budigle.
“Hatua hii inawavunja
moyo wawekezaji katika sekta ya elimu. Hawa ni wadau katika elimu na ni vizuri TCU wakatuchukuliwa hivyo. Wao ni
wasimamizi ambao wanatakiwa kuwaongoza na kuwarekebisha pale wanapokosea.
Kitendo cha kukifutia vibali bila kufuata haki kinawavunja moyo wadau wa elimu
pamoja na wanafunzi pia,” aliongeza Budigle.
Akitangaza hatua hiyo hivi
karibuni Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alizitaja sababu
za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya muda mrefu baina ya
uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji wake
kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.
4 comments:
Jengo ulilotumia siyo la st Joseph ni la SAUT MWANZA,Liondoe kuondoa mkanganyiko kilichofungiwa ni st joseph siyo st. augustine
Nakubaliana na wazazi wote hapo juu, kwani yaelekea hawa TCU hawajui wanalolifanya. In facts, historically religious institutions have been the best providers of education in Tanzania. Rais JPM needs to overhaul the whole TCU board. Wanatuharibia mfumo wetu wa Elimu. Wanataka kila mtanzania asome kwenye hizo public institutions za DSM, UDOM, SUA, n.k.? Serikali lazima iingilie kati na kuviruhusu hivi vyuo vifunguliwe na kama kuna dosari, basi wapewe muda wa kuzirekebisha. Licha ya kuwanufaisha wanafunzi kielimu, kuwepo kwa vyuo hivyo vinasaidia ajiri kwa wananchi wa miji hiyo miwili. Therefore, it is an educational as well as an economical issue. Mtukufu Rais JPM, tunakuomba tumbua haya majibu pale TCU.
Ww haujui matatizo ya st.joseph
Ww haujui matatizo ya st.joseph
Post a Comment