Stars inatajia kucheza mechi hiyo ya marudiano ikiwa na faida ya bao 1-0 walililopata ugenini, shukrani kwa Samatta Mbwana aliyefunga bao hilo.
Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto alisema jana kuwa Waziri Mkuu Majaliwa ametuma salamu za pongezi kwa wachezaji wa Stars na kuahidi kuja kushuhudia mchezo huo wa marudiano.
"Waziri Mkuu amewapongeza wachezaji wa Stars kufuatia ushindi walioupata ugenini katika mechi ya kwanza.
Ameahidi kuungana na mashabiki wa soka kwenye mechi ya kesho," alisema Baraka akimnukuu Majaliwa.
Katika mchezo huo, waamuzi kutoka Djibout ndiyowatakaochezesha; Djamal Ade Abdi, Abdillahi Mahamoud Iltireh, Farhan Bogoreh Salime.
Kuhusiana na viingilio, alisema kile cha juu kitakuwa Sh. 25,000, wakati VIP B,C kiingilio kitakuwa Sh. 20,000 na kiingilio cha chini kabisa kitakuwa Sh. 5,000.
Kuhusu maandalizi, alisema kikosi kinaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa chini ya Kocha Boniface Mkwasa.
"Wachezaji wote wako kwenye hali nzuri, Kelvin Yondan na Mwinyi Kazimoto nao wamepata nafuu kutokana na maumivu waliyopata," alisema Kizuguto.
kadhalika, Mkwasa amemuongeza mchezaji, Adiblah Yusuphambaye tayari ameshaungana na wenzake kwenye mazoezi.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment