ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 27, 2016

CHAD YAJITOA, CAF YAIFUNGIA HADI 2021

Shilikisho la Soka Barani Africa, CAF imetangaza kuifungia nchi ya Chad kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa, AFCON mpaka mwaka 2021 na kuipiga faini ya dola 20,000 kwa kujitoa michuano ya AFCON 2017, hivyo itafungiwa AFCON 2019.

Kutokana na kujitoa kwao, mechi yao ya kesho Jumatatu March 28, 2016 dhidi ya Tanzania haitokuwepo tena. 
Na kwa mujibu wa kanuni za mashindano za CAF, timu itakayojitoa kwenye kundi hatua ya kufuzu, basi matokeo yake yote yatafutwa.

Matokeo ya ushindi wa 1-0 waliopata Tanzania kule ugenini yamefutwa na Tanzania sasa itabaki kuwa na point 1 tu. Kwa maana nyingine, kinara wa kundi G pekee ndio atafuzu AFCON 2017 tofauti na awali ambapo timu ya pili ingefuzu mtoano.

No comments: