Bi.Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle
cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo, lakini
matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete kutetea wagonjwa
wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kumuomba
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati mpango wa kuwaondoa wagonjwa
6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye hospitali wanakotoka.
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, MNH, na
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa
msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu),
waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.
Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu
“Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala
Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Hospitali hiyo, Profesa Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi
wa habari leo Aprili 25, 2016.
Hofu ya wagonjwa
Awali
baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na
Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa
jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini
hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye
utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali
walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.
Gharama za matibabu ya Selimundu
Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa
ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu, Mradi huu
kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa
ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi
wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji
yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Amesema
Profesa Mseru.
Naye
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt.Doroth Gwajima, amewaondoa
hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema, muongozo wa
serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure na wengine
wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata hivyokwa wale ambao
hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu upo.
Hofu ya wagonjwa
Kutokana
na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa selimundu,
na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa huo, wagonjwa
wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo?
Wazazi wa watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli,
kuingilia kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya
ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya viungo, na
wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.
Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
“Hospitali
zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo mikoani na
wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu, na hata
ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa huandaliwa na mgonjwa
hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili kupatiwa matibabu yanayofaa.” Dkt.Grace
Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.
Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu
Bi.Mkami Titus wa Temeke jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake Shedrack Yahaya(4), anayeugua selimundu
Bi.Walivyo Mohamed kutoka Rufiji mkoani Pwani, akiwa na mtoto wake wa miaka 4, Siraji Majid
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitaliya Taifa Muhimbili, (MNH), Profesa Lawrence Museru, (kulia), akiwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa na Afya ya Watoto ya MNH, Dkt. Mary B. Charles, akizungumza na waansdishi wa habari wakati akitoa taarifa yake mapema leo Aprili 25, 2016
Profesa Museru
Dkt.Doroth Gwajima, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto
Profesa Museru natimu yake wakati akiongea na waandishi wa habari
Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Elineema Meda. Dkt. Meda ni mmoja wa walioshiriki kwenye utafiti wa ugonjwa huo wa Selimundu chini ya mradi wa Welcome Trust
Bi. Yasmin wakati wa mkutanona waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
Baadhiya akina mama wakiwa na watoto wao wanaosumbuliwa na maradhi ya Selimundu. Hapa wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Bi. Yasmin ambaye ameamua kuwasimamia na kuwasemea wagonjwa wa Selimundu
Bi. Yasmin (katikati), akiwa na Bi.Walivyo Mohammed na mtoto wake Siraji (kushoto) na Bi. Getrude Thadeona mtoto wake Angela
No comments:
Post a Comment