ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, April 7, 2016

TAARIFA KWA UMMA: KUFUTWA KWA SAFARI ZA NDEGE APRIL 2, 2016



Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.

Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa taa kwenye njia ya kurukia kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na hivyo kukosekana kwa usalama ambao ungewawezesha marubani wetu kutua.

Huu ni mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kufutwa kwa ndege mbili miongoni mwa ndege zetu kutua usiku ule:

Ndege Na. FN157 iliondoka kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda unaotakiwa saa 4.40 usiku. Wakati ndegte ikikaribia Uwanja wa Kilimanjaro marubani wetu walijulishwa na mnara wa kuongozea ndege kwamba taa zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa muda usiokuwa mrefu. Ndege ilizunguka uwanja wa Kilimanjaro ikisubiri ukarabati wa taa hizo kwa takribani dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi.
Ndege iliwasili tena Dar es Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye ukumbi wa kusubiria ndege wakati ndege ikijazwa mafuta tena na marubani wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari kurudi Kilimanjaro mapema kadri iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia ndege ukikamilika. Kwa bahati mbaya taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi hadi kufikia saa saa 7.00 usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016, ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa walishakuwa kazini kuanzia saa 12.30 jioni.
Hii inamaanisha kwamba hatukuwa na mbadala wa kufuta safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo ilikuwa irudi kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam.
Abiria wetu waliopata usumbufu walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia na ilisafiri kutoka uwanja wa pili kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira walichukua mbadala huu lakini wengie waliamua kubaki katika uwanja wa ndege kusubiri ndege iliyofuata.
Abiria wote walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege iliyofuata walisafiri nasi kwa kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016.
TAARIFA KWA UMMA:
Tunaomba radhi kwa abiria wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu walioupata huku tukiwahakikishia kuwa tunaweka kipaumbele kikubwa kwenye usalama wa abiria wetu na marubani.

John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet Tanzania

1 comment:

Anonymous said...

Hawa FastJet business yao ni ngumu mno. Ndege zinakuwa delayed several times, upon delay walitakiwa wawaambie abiria wao na kuhakikisha wamewapa huduma maalumu. Imagine wamewalaza watu airport. According to my little understanding walitakiwa wanawapa watu accommodation and any other necessity wakiwa wana delay ama cancellation of the flight by last minute. I think they need to re-review their services.

Tulijua kwa kuwa wanaitwa Fast, na huduma zao zingekuwa solid, wasibabaishe kama wale companies wengine. To tell you the truth, Air Tanzania itakaposimama in it's services, watu wengi sana tutawakimbia kama ukoma. Unless otherwise they review their services. Na hata ukiisoma hii habari, they're covering up their stupidity.