( Picha vijana wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Iringa Richard Kasesela (hayupo pichani) leo asubuhi.
Nafasi za kuingia JKT zimekuwa changamoto kubwa sana. Wilaya ya Iringa wamejitokeza zaidi ya vijana 612 kuomba nafasi za kujiunga na JKT. Nafasi zilizopo kwa wilaya nzima ni 100 tu. Zoezi la kusaili vijana linaendelea hadi jumatano. baadae Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mwenyekiti wake Richard Kasesela itakaa jumamosi kuchagua majina ya vijana hao. Mwitikio huu unaonyesha ipo haja ya kuongeza idadi inayotakiwa kwa vijana kwenda kwenye mafunzo ya hiari ya JKT.
No comments:
Post a Comment