Advertisements

Monday, May 30, 2016

MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI PAPUA NEW GUINEA KUMUWAKILISHA RAIS MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Belize Bw. Wilfered Eliringron wakati Makamu wa Rais alipowasili katika Hoteli ya Airways mjini Papua New Guinea. Makamu wa Rais yupo Nchini Papur New Guinea kwa ajili ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho utakaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutano huo utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwandaaji Mkuu wa mkutano wa The HL MEETING UN WOMEN unaotarajiwa kufanyika keshokutwa mjini Guinea, Makamu wa Rais Makamu wa Rais yupo Nchini Papur New Guinea kwa ajili ya kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho utakaojadili masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa. Mkutano huo utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP). (Picha na OMR Papua New Guinea).

1 comment:

Anonymous said...

Hii mikutano ya kuhadili namna ya utekelezaji wa malengo ni danganya toto tu. Leo hii hakuna asiyejua cha kufanya kutekeleza. Kinachohitajika ni fedha tu. Waliotunyonya siku nyingi leo hawana fedha. Hiyo inayodaiwa kuwa eti ni misaada hata kwao huko matatizo kibao. Hivi tunahitaji safari kama hii ya kujadili eti "masuala ya kukuza Usawa na Maendeleo endelevu kwa ajili ya Wananchi wa Nchi wanachama kuimarisha majukumu ya Nchi za ACP katika Utawala Bora na Maendeleo, Usalama na Utulivu wa kisiasa" Huhitaji kuwa Profesa kujua majibu ya hilo. Ndio maana Rais Magufuli amefanya vyema kutohudhuria makongamano haya ya maneno tupu. Fedha ya safari hii ingejenga shule ya msingi ama kulipia waalimu wa wanafunzi kule UDom. Hebu tubadilike tumsaidie Magufuli na tuisaidie nchi yetu. Sio kila kitu Magufuli pekee ndio apige kelele.