ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, May 11, 2016

SEREKALI YATAKIWA KUAJIRI NA KUPELEKA WAGANGA ,WAUGUZI NA WAKUNGA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika Mkutano ulio fanyika katika ukumbi wa CCM mkoa lakini pia katika Mazungumzo yake alimtaka ,Mstahiki Meya kutopokea hongo za wapinzani ili kujiuzuru alisema ''MSTAHIKI MEYA TUNATAMBUA CHAMA CHA CUF KINATAKA KUKUPA HONGO ILI UJIZURU NAFASI HIYO NNAKUTAHADHARISHA KAMWE USIJARIBU KUKICHEZEA CHAMA CHA MAPINDUZI NA SISI KAMA VIJANA WA CCM TUNAKUTAKA KUPUUZA YOTE NA KUFANYA KAZI BILA VISHAWISHI VYOVYOTE ILI TUFIKIE MALENGO YA KUITEKELEZA ILANI YA CCM 2015-2020 UCHAGUZI UMEKWISHA SASA NI MUDA WA KAZI''
Wanachama Wapya Wakila kiapo cha Chama na Jumuiya
Na Woinde Shizza, Tanga

Serikaki umeshauriwa kusomesha , kuajiri na kupeleka waganga, wauguzi na wakunga katika maeneo ya vijijini ili ukokoa maisha ya kina mama wajawazito, iiiweko kutoa huduma bora za afya na tiba .

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM )umetoa ushauri huo baada ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kutembelea hospitali kuu ya Bombo katika Manispaa ya Mji wa Tanga.

Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alitoa ushauri huo alipomaliza kutembelea hospitali hiyo , kusikiliza kero , kupata maelezo toka kwa muuguzi wa zamu Atose Kiluvia katika hospitali ya Bombo mkoani hapa .

Shaka aliueleza Muuguzi Kiluvia amueleze mganga mkuu wa wilaya kwamba ili kufikia malengo ya mil enia kuna ulazima wa kuhakikisha maisha ya kina mama wajawazito yanawekewa utaratibu bora wa kudumu ili kunusuru maisha yao , kupata ushauri wa maendeleo yao nyakati za ujauzito wakipata huduma katika vituo vya huduma ya afya.

Alisema ili huduma hizo ziweze kuimarika na kutolewa kwa wakati, mkakati pekee ujaohitajika na kupewa kipaumbele ni kuweka mazingira bora kuanzia halmahsuri za wilaya hadi serikali kuu ili kusomesha, kuajiri na kupeleka wakunga, waganga na wauguzi maeneo ya vijijini.

"Mikakati ya maendeleo ya uimarishaji huduma za msingi za kijamii ziibuliwe katika ngazi za halalmshauri za wilaya kabla ya Serikali kuu haijaweka mkono wake, madiwani na wakurugenzi wa halmashauri watenge muda wankushughulikia nw kuondosha kero mapema" alishauri Shaka.

Alisema haiwezekani madiwani wakashiriki vikao vya Baraza la madiwani ambalo ni bunge la wilaya bila kujadili huduma zznjamii lama vike ujenzi wa vituo vya afya, masuala ya kilimo, mifugo, miundombinu au ajira za wakunga, waganga na wauguzi.

Aidha alisema haiwezekani kuzungumzia mpango wa maendeleo ya nchi huku kukiwa na hali ya kuzorota kwa huduma za jamii kama tiba , chanjo na kinga au kuwepo upungufu wa wauguzi, wakunga na waganga .

"Zijengwe nyumba bora za kisasa ambazo waganga, wakunga na wauguzi wataishi na kuridhika, walimu na wataalam wengine wa maendeleo ya kiseta pia wawe na nyumba za uhakika maeneo ya vijijini. "Alisema

Halmashauri ikipeleka umeme, zikajengwa barabara, nyunba za wataalam wetu , hakuna atakayekataa kuishi vijijini, siasa ya ujamaa na kujitegemea haina maana watu waishi katika nyunba za nyasi, hata mkienga nyumba za roshani bado mtabaki kuwa wajamaa.

Alisema serikali kuu haiwezi kufanya kila kitu katika vitongoji, vijiji, kata na kwenye wilaya,kazi hiyo lazima ifanywe na halmashauri zetu wakiwemo wataalam na madiwani.

"Kazi ya serikali kuu ni kupeleka ruzuku, fedha za ruzuku zisitafunwe na mchwa , kazi ya madiwani ni usimamizi wa matumizi bora ya fedha za umma, yakipatikana mafanikio kila kijiji ndiyo maendeleo ya Taifa "alisema Shaka ambaye emeanza ziara ya siku sita mkoani hapa.

No comments: