Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya matukio ya kialifu katika jiji la Dar es Salaam ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu walivyokamata kwa Wenceslaus Mtui anayedaiwa kuwa ni tapeli ya madini bandia leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro akionyesha baadhi ya vitu walivyokamata kwa Wenceslaus Mtui anayedaiwa kuwa ni tapeli ya madini bandia leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linashikilia mkazi wa Makongo, Wencelaus Mtui anayedaiwa kuhujihusisha na utapeli wa madini kwa kumtapeli mtu na kisha madini bandia yenye thamani ya Sh.Milioni 90,000.
Akizungumza na waandishi habari leo Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina (CP),Simon Sirro amesema kuwa mtu aliyetambeliwa kiasi cha fedha hizo alilipa kupitia benki ya CRDB kwa madini bandia ya dhahabu Kilogram 20 zenye thamani ya Dola za Kimarekani 40,000.
Amesema baada ya mtu huyo kulipa fedha hizo alikabidhiwa vipande vitatu vya madini venye uzito wa Kilogram 212 na kugundua kuwa ni madini bandia.
Jeshi la polisi lilipompekuwa ofisini kwake na nyumbani kwake walimkuta ,Chuma cha kuchomea madini,Mashine ya kupima madini ,vifaa vya kubania (Seal 53) pamoja na taarifa mbalimbali za malipo ambayo ameweka benki na kutoa.
Mtui ambaye anadaiwa kuwa ni tapeli wa madini pandia anamiliki kampuni ya Crown Logistics and Cargo Handling Limiited.
Wakati huo huo jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linamskilia Waziri Jamal (39) mkazi wa Mbezi Msakuzi ambaye wamemkamata na silaha moja aina ya Bastola Browning 6.35 Calbre yenye namba za usajili A.08416/ Car 90522 na baada ya kumhoji wameweza kubaini mtandao wao wa watu nane.
Aidha jeshi la polisi limesema kuwa askari aliyeuawa jana kwa kupigwa risasi ni wa mkoa wa pwani na kuahidi lazima watakamatwa wote waliohusika.
No comments:
Post a Comment