Advertisements

Wednesday, May 18, 2016

VIDEO: SHILOLE NA VANESSA MDEE WAMEINGIA KWENYE BIFU ZITO.

Bado kisa na mkasa hakijabainika wazi lakini ni Shishi ndiye aliyeanza kumtupia maneno Vee Money kwenye Instagram. Kuna uwezekano mkubwa wawili hao walizinguana nyuma ya pazia kabla ya kuamua kuumwaga ubuyu mtandaoni.

“Vee Jipange sana mwenzio Igunga niliaga sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge,” aliandika Shilole kwenye post ya Instagram ambayo imefutwa tayari. “We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga, mi ndio mtoto wa mbwa sasa maninaa,” aliongeza Shilole.

Vanessa hakukaa kimya, alimjibu Shishi kwa post ambayo aliifuta muda mfupi baadaye. Akipost picha ya Shishi, Vee aliandika: Nikupe Kickiii ujulikane au sio? Kila siku twanyamaza ndio mtugaraze. Sit the f*ck down. Mimi sio wale uliowazoea. Ps: You ain’t worth this post inashushwa sasa hivi #MessageSent.”



Haijashia hapo. Shilole amepost video akimpa ujumbe mwingine mkali zaidi muimbaji huyo wa ‘Niroge.’

“Vanessa nimepata ujumbe wako wa Kiingereza japokuwa nimeusoma kwa tabu sana lakini nimepata baadhi baadhi,” anasikika akisema kwenye video hiyo.

“Listen to me my sister, you see me nah, mimi mwenzio nimezaliwa Igunga, nimezoea kula ugali, sijazoea kula chips mayai kama unavyokula wewe. So mama ninapiga kuliko maelezo, usiombe kukutana na mimi, au waulize wenzio waliokutana na vibao vyangu wanaweza kukuambia kwamba kibao cha Shishi ukikutana nacho lazima uombe Panadol,” anaonya Shishi.

“Aisee bibi, bibie, bibie, I am telling you yaani usiombe kukutana na Bi Shishi, yaani usiombe ukakutana na mimi tit for tat, yaani mama Kiingereza chako nimekiona, jipange, I am telling you, If I see you, me and you.”

Acha tuone movie hii itaishia wapi. Lakini kwa vitisho hivyo Vanessa hana budi kuwa na bodyguard wake sasa.

4 comments:

Anonymous said...

Wewe shishi acha mihasira ya kujinga unafanya mambo ya kitoto ss ukikutana nae ndio umpige? acha utoto shishi celebrity mkubwa kama wewe huo muda wa kujirekodi mahasira ungetumia kurekodi paka la bar part 2

Anonymous said...

if I see you eeeh, I am telling me! hahahahahahahahahahaha

Anonymous said...

Acha ushamba wee shishi ..grow up..eti nitapiga vibao...unafikiri sifa hio? Ninkujishusha hadhi..hufugiki..issue kila siku ..komaaa kizungu hujui ndo tena wewe ndo unaunga unga balaa

Anonymous said...

Huyu shishi uswahili umemjaa tele,elimu zero,kiingereza zero bora uwe unaongea fluent swahili utaeleweka zaidi,unapenda ugomvi sana sio fresh,kuwa mstaharabu,sasa unataka kumpiga Vee then utafaidika nini????mweee,tupelekeni watoto shule jamani,SMH