Advertisements

Saturday, June 18, 2016

JK AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip Mangula mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya CCM ofisi ndogo, Lumumba muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati kuu maalum. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia ajenda kabla ya kikao kuanza kwenye ukumbi wa NEC , Makao Makuu ya CCM ofisi ndogo kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum kilichofanyika Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika , Makao makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba

No comments: