Advertisements

Monday, June 20, 2016

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA KITUO CHA UHAMIAJI HOLILI

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (katikati), akikagua mzigo wa John Evarist ambaye ni mfanyabiashara aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yuko mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Mfanyabiashara John Evarist aliyekua akipita kutoka nchini Kenya kupitia mpaka uliopo katika kijiji cha Kamkunji, mkoani Kilimanjaro, akijibu maswali aliyoulizwa na Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea(wa kwanza kushoto).Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyepo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini
Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji Holili, ACI Kagimbo Hosea ( aliyenyoosha mkono), akimuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto), mwisho wa mpaka unaotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya wakati wa ziara ya Katibu Mkuu kukagua njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.Wa pili kushoto ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, RPC Wilbrod Mutafungwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira (kulia), akipanda Mlima kwenda kukagua jiwe linalotenganisha nchi ya Tanzania na Kenya katika Mpaka uliopo eneo la Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.
Ujumbe ulioongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(), ukishuka kutoka mlimani baada ya ukaguzi wa mpaka uliopo Mlima Nyoka, mkoani Kilimanjaro. Katibu Mkuu yupo mkoani Kilimanjaro katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua na kudhibiti njia zinazotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI



No comments: