Tuesday, June 14, 2016

KKKT Kihesa wavuna 8,950,000 katika changizo liliongozwa na Mkuu wa Wilaya

Tarehe 11/06/2016 Mkuu wa wilaya alikuwa Mgeni rasmi katika changizo la kwaya Kuu ya KKKT Kihesa hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Iringa. Iliongozwa na baba Askofu O.M. Mdegela. Kiasi cha shilingi 8,950,000 zilichangishwa. Mungu alitenda muujiza wa utoaji. Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya aliomba sana wakristo waliombee taifa hasusani Wilaya ya Iringa ambapo watoto wamekuwa wananyanyaswa sana kijinsia. Baba askofu katika mahubiri yake aliwaomba waumini kuimba nyimbo kwa staha na pia kuangalia ni nani wanaye mwmbia. hafra hiyo pia ilihudhuriwa na wakuu wa majimbo na wachungaji pamoja na viongozi wengine wa serikali na vyama. (Kwa habari zaidi pia tembelea IRINGA DC FACEBOOK PAGE)​

No comments: