Advertisements

Thursday, June 23, 2016

MBUNGE WA JIMBON LA KIKWAJUNI MHANDISI HAMAD MASAUNIN AKABIDHI JEZI ZA MASHINDANO


Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi nahodha wa timu ya Mkunazini, Ahmed Omari Haji , jezi zitakazotumiwa na timu yake wakati wa Kombe la Masauni -Jazeera, linaloanza kutimua vumbi leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Zanzibar. Wapili kulia ni Diwani wa kata ya Miembeni, Mbaruku Abdallah Hanga.

Nahodha wa timu ya Kikwajuni Bondeni, Salum Said (kushoto), akipokea jezi kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia).
Muonekane wa nyuma wa moja ya jezi zitakazotumiwa katika mashindano ya kombe la Masauni/Jazeera , kutoka maeneo mbalimbali katika Jimbo la Kikwajuni kama inavyoonekana.

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, ambae pia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto), akiwa na baadhi ya viongozi na makocha wa timu zinazotarajiwa kuanza kumenyana katika mashindano ya Kombe la Masauni-Jazeera, muda mfupi baada ya kukagua Uwanja wa Mnazi Mmoja utakaotumika kwa mashindano hayo.(Picha na Mpiga Picha Wetu)

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambae pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekabidhi vifaa vya michezo ikiwemo jezi na mipira kwa manahodha wa timu kumi zinazotarajiwa kushiriki mashindano yaliyopewa jina la Masauni - Jazeera CUP 2016, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika ofisi ya Jimbo la Kikwajuni

Akizungumza kabla ya kutoa vifaa hivyo vya michezo, Mhandisi Masauni alisema lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kuwafanya vijana wawe na afya pamoja na kujiepusha kuwa katika magenge mabaya ambayo yanaweza kusababisha kijana kushawishiwa kujiingiza katika matendo ya uhalifu huku ikiwa ni moja ya ahadi aliyohaidi wakati wa kipindi cha kampeni kuboresha michezo katika jimbo hilo

“Vijana ni nguvu kazi ya Taifa lolote lile duniani linalotaka kupiga hatua katika sekta ya maendeleo, lengo la mashindano haya yanayoenda kuanza leo ni kuwaepusha vijana kujiingiza au kushawishiwa kushiriki matendo ya uhalifu ikiwa pamoja na kulinda afya zao,” alisema Masauni.

Mmoja wa manahodha wa timu zilizokabidhiwa vifaa hivyo, Salum Said alisema wanawashukuru wadhamini wa kombe hilo ambao ni Mbunge wa Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na Mwakilishi wa Jimbo hilo Nassor Salim Jazeera kwa kutambua uwepo wa vijana huku akiahidi timu yake ya Kikwajuni Bondeni kuwa bingwa wa ligi hiyo.

Mashindano hayo yatatanguliwa na mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha timu ya Maveterani wa Jimbo la Kikwajuni na Kundi la G1.

MWISHO……

No comments: