Advertisements

Friday, June 17, 2016

WABUNGE WENGINE WASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO LEO JUNE 17 2016

Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest.

Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu.

Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

2 comments:

Anonymous said...

mkiambiwa ukweli mnasimamisha watu kuhudhuria ila lisemwalo lipo...sijui lini nchi yetu itakuwa huru kwenye kila sehemu

Anonymous said...

Watu waliozoea siasa za matukio,na kuvizia kashfa si rahisi kuperfom kwenye mijadala ya kistaarabu.Unapokuwa mbunge na kushindwa kureserch information ulionayo kama ni factual kabla hujaiwakilisha bungeni unakuwa na dhamira ya upotoshaji hivyo ni bora wakaungane na wanaharati wenzao wanaosubiri hatma ya kesi yao na polisi.