Advertisements

Saturday, June 18, 2016

Yanga wakiwasili mjini MO Bejaia hapo jana, wenyeji wao klabu ya MO BejaiaYanga wakiwasili mjini MO Bejaia hapo jana, wenyeji wao klabu ya MO Bejaia waliandaa mabasi mawili madogo aina ya Coaster lakini kwa tahadhari Yanga tayari mapema walikuwa wameandaa basi lao kubwa kwa ajili ya kuwabeba wachezaji kisha Coaster moja ikawabeba viongozi iliyobaki tukawambia rudisheni.Msafara ukaelekea hotel ya Raya iliyopo Bejaia.


Usiku wa leo saa 6 kwa saa za hapa Tanzania kikosi cha Yanga kilifanya mazoezi kuzoea changamoto za uwanja pamoja na hali ya hewa kutegemeana na muda husika wa mchezo huo.

KIUNGO Mshambuliaji Obrey Cholla Chirwa ameondoka alfajiri ya leo kuelekea Algeria kuungana na timu yake mpya Yanga SC iliyopo nchini Algeria.

Baada ya kukamilisha usajili wake tayari klabu ya Yanga imetuma CAF jina la mchezaji huyo ili kupata leseni yake, ni mategemeo kuwa leseni ya Chirwa itafika jioni ya leo!Mzambia huyo anayechezea timu ya taifa ya Zambia chini ya miaka 23 kwa mara nyingine ataonana na pacha wake wa zamani katika safu ya ushambuliaji ya FC Platinum Donald Dombo Ngoma.

KILA LA HERI OBREY CHOLA CHIRWA.

No comments: