Advertisements

Monday, July 11, 2016

Daktari feki akamatwa hospitali ya rufaa Morogoro

By Lilian Lucas Na Hamida Shariff,Mwananchi Mwananchipapers@Mwananchi.co.tz

Morogoro. Mtu mmoja, Zakaria Benjamin(35) mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kuingia na kufanya Udaktari katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro wakati hana taaluma ya udaktari.

Daktari huyo feki inadaiwa aliingia katika hospitali hiyo ya rufaa Julai 10 mwaka huu majira saa 10 alfajiri huku akijifanya kukagua na kutembelea wagonjwa katika wodi mbalimbali hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akizungumza na waandishi wa habari jana alisema daktari huyo aliingia hospitalini hapo isivyo halali kwa nia ya kutaka kuiba.

Matei alisema daktari huyo aliotembelea wodi namba 1,7 na 9 na kujifanya kuwa yeye ni daktari mgeni hivyo anakagua wagonjwa kuona kama wamepata huduma ipasavyo.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa huyo alipofika katika wodi namba 7 alienda katika chumba cha kubadilishia nguo kisha kuvalia koti la kidaktari lililokuwa limeegeshwa mahali hapo.

1 comment:

Anonymous said...

Unaweza kutafakari ni jinsi gani hakuna ulinzi madhubuti na pia wafanyakazi kujuana? Ina maana wodi zote alizotembelea hakuna usimamizi wa Nurse supervisor au Daktari muangalizi. Hadi akabadili nguo.? Swali kubwa angelikuwa gaidi wa kutega bomu ingekuweje? Tuweni.makini kwenye jamii na hasa kama.hospitali sio wote watakaoweza kukimbia hata mahali pa kujiokoa kwani ni wagonjwa. Tatizo kubwa nililoliona kwa walinzi wa Tanzania ambao wanatoka kwenye makampuni binafsi hawako smart kimkagua mtu na kuuliza maswali ya kiuchunguzi wamekaa kuchoka kwenye kitu muda wote wa kazi na hadithi nyingi tu ! Unaweza kumpita mlinzi yuko anasoma gazeti!?