Advertisements

Sunday, July 10, 2016

HALI BADO TETE SUDAN KUSINI

Rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar wamewasihi wafuasi wao kulinda amaniWanajeshi wanamuunga mkono makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar wanasema kuwa kambi yao imeshambuliwa usiku wa kuamkia leo kwa risasi na bunduki nzito nzito.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini unasema kuwa kumetokea ufyatulianaji wa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba..

Maeneo yanayodhaniwa kuathirika sana ni yale ya Jebal.

Ujumbe huo unasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa rasasi ulishuhudiwa karibu na kambi ya umoja wa mataifa

Siku za hivi majuzi ziaidi ya watu 100 wanaripotiwa kuuawa mjini Juba wakati wa mapigano kati ya wafuasi wa rais Salva Kiir na makamu wa rais Riek Machar

Wawili hao walikubaliana kumaliza vita vya wenywe kwa wenyewe na wametoa wito wa kuwepo utulivu.

Ripoti za awali kutoka nchini Sudan Kusini zilisema kuwa takriban watu 100 waliuawa wakati wa mapigano kati ya wanajeshi hasimu katika mji mkuu Juba.

Hata hivyo idadi kamili bado haijulikani lakini wengi wa wale waliouawa wanaripotiwa kuwa wanajeshi.

Mapigano hayo yaliyoanza siku ya Alhamisi yaliendelea hadi mapema Jumamosi.

Mwandishi wa habari mjini Juba anasema kuwa wanajeshi wameweka vizuizi vya barabarani mjini humo.

Anasema kuwa masoko yamefunguliwa lakini watu wengi wamebaki nyumbani.

Sudan Kusini inaadhimisha miaka mitano ya uhuru wake.

BBC

1 comment:

Anonymous said...

Hapakuwa na sababu ya kukimbilia kuingiza South Sudan katika east African community ihali wao wenyewe hawajitambui wala kuthamini uwepo wao kama nchi.