Advertisements

Monday, July 25, 2016

MAHAKAMA KUU KANDA YA IRINGA YAMTIA HATIANI MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANAHABARI MWANGOSI

 Ulinzi  wa  polisi  viwanja  vya mahakama  kuu kanda  ya  Iringa  leo  kabla ya  mtuhumiwa wa mauwaji  kufikishwa.
 Wananchi  wakiwa  foleni  kukaguliwa  kabla ya  kuingia  mahakamani leo.

 Mtuhumiwa wa  mauwaji  ya  Mwangosi  akipakiwa  kwenye  gari  za  FFU
 Msafala  wa  gari  za  FFU  zilizomsindikiza askari  mwenzao anayekutwa  na kosa  la  kuua bila  kukusudia  leo
 Askari  wa FFU  wakitoka  mbio  mahakamani  hapo
 Wananchi  na  wanahabari  wakitoka  mahakamani  hapo 

Wakili  kutoka mtandao  wa  watetezi wa haki  za  binadamu ((THRDC), Benedict  Ishabakaki  akizungumza na  wanahabari  nje ya  viwanja  vya mahakamani  leo
 Askari  hao  wakimtoa mahakamani  hapo  leo  mtuhumiwa wa mauwaji ya  Mwangosi

Na  MatukiodaimaBlog Iringa

 MAHAKAMA   kuu  kanda  ya  Iringa   imemtia hatiani   kwa   kosa la  kuua bila  kukusudia  askari  Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU )Iringa  G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa  kuuua  mwaahabari  Daudi  Mwangosi   mwaka 2012 katika  kijiji  cha  Nyololo  wilaya ya  Mufindi.

Hata   hivyo  mahakamani  hiyo  imesema  adhabu  kwa  mtuhumiwa   huyo  kutokana  na kupatikana na  kosa  hilo la  kuua bila  kukusudia  itatolewa  Julai 27  majira ya  saa 4  asubuhi  mwaka   huu.


 Jaji  Dkt  Paul Kiwelo ambaye  anayesikiliza  kesi  hiyo alisema  mahakakamani hapo jana   kuwa kati  ya  vielelezo  vitano vyote  vilivyoleta  kama  ushahidi  mahakamani  hapo  kwa ajili ya  kesi   hiyo  namba 54 ya  mwaka 2013  ni  kielelezo   kimoja  pekee  cha  ungamo  kwa  mlinzi  wa amani  ambacho  ndicho  hakukuwa na  shaka   na ungamo  hilo  ndilo  lililomtia hatiani  asikari  huyo.


Alivitaja   vielelezo vilivyopelekwa kama  ushahidi   kuwa ni Ramani   ya  eneo la  tukio,ripoti  ya  tabibu ,ungamo  la mlinzi  wa amani ,silaha  aliyoitumia  na  rejista  ya  silaha.

             

No comments: