Advertisements

Monday, July 18, 2016

MAKONDA AWATOLEA UVIVU WANAOMBEZA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , paul Makonda akizungumza ndani ya Power Breakfast ya Clouds Fm 
Na Mwandishiwetu, Dar es Salaam

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameamua kuwavulia uvivu wale wote wanaosambaza ujembe wa tofauti juu ya maagizo yake katika mitandao ya kijamii.

Makonda ambaye aliamua kutenga muda na kuelza maswala kadhaa yausuyo jiji la Dar es Salaam kupitia kipindi cha Power Breakfast ya Clouds Fm na 360 ya Clouds Tv juu ya watu ambao wanaotengeneza account feki za mitandao mbalimbali kupitia jina lake.

“Kwanza wanapaswa kujua kuwa sina account ambayo inanza na cheo cha ngu hivyo account zote zangu zimeandikwa kwa jina langu Paul Makonda sio vingine hivyo kila mtu anapaswa kuwa makini na hilo” anasema Makonda.


Anasema kuwa juu ya agizo batili lililopostiwa katika mitandao ya kijami kuwa wasikuwa nakazi kwamaba watakwenda jela sio la account yake bali yeye ameagiza wenyeviti wa serikali ya mtaa kuhakikisha kuwa wanafanya uhakiki wa wakazi wao nyumba kwa nyumba kwa ajili ya usalama wa Maeneo wanayokaa.

Anataja kuwa kutokana matatizo yaliyopo kamwe ataocha kupambana na mafisadi katika Halmashauri zote tatu,wauza unga , wafanya biashara wa Shisha na Mashoga.

Hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huu kuwa makini na kufata maelekezo ya wenyeviti mitaa amabayo nimewapa hili tuweze kuimarisha ulinzi kuanzi ngazi ya chini kabisa.

mwisho

2 comments:

Anonymous said...

Asante mkuu ila ujue hii kazi ni nzito sana na ilishaagizwa na mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema wakati huo naibu waziri na waziri pia kuanzishwa kwa Sungusungu!. La ajabu hebu tafakari kwaza utitiri wa wanajamii wanaofurika mjini kote siku nzima je wanalala wapi? utakuta chumba kimoja kina watu zaidi ya 5! na hii yote pia wanasaidiana kulipa kodi tokana na uwezo na kazi walizonazo!
Kuna utaratibu pia unaofaa kama alivyodokeza Meya wa Jiji, hivyo la msingi ni kukaa pamoja na kulitafutia ufumbuzi kwani kwenda kwenye vyombo vya habari na kupaaza saUTI bado hakujatatua tatizo! Uongozi wa serikali za mtaa umelega sana tukitizama maeneo mengi hata eneo la barabara ni mbovu linapitika kwashida, bomba la maji limepasuka maji yanatawanyika hovyo, lakini la ajabu hawawezi kuwaunganisha wananchi wa eneo husika walau siku za Jumamosi kurekebisha maeneo yao.
Wewe kama mkuu wa Mkoa jiji kuu DAR, je ulishapita (na kama bado naomba upite)barabara ya kutoka Sinza kijiweni kuja Magomeni kupitia kwa Mtogore, kweli hii barabara inatia aibu na maji machafu pembezoni isitoshe biashara nyingi magari mabovu yamejaa kila eneo pembezoni mwa barabara na huu ndio Mkoa wako mkuu! Isitoshe ulikuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ya Kinondoni! Haya ndio mambo ya kuangalia sana pia kwa afya za watu, Kwa ushauri tu ni vyema ukaomba serikali ikatoa eneo kama kule Chalinze ndani likatengwa kwa ajili ya magari mabovu yaliyojaa mitaani na liwe maalumu kwa kila mwenye gari bovu alipeleke huko mwenyewe na kupewa namba maalum hivyo akitaka kupata spea aende kuchukua huko kuendana na namba na plot gari bovu lake liliko. ushauri tu.
kuna mambo mengi ya kulifanyia jiji letu na sio kuonekana kwenye vyombo vya habari tu!! Tufanyeni kazi kwa ushirika sio kudharauliana. Mwisho.

Anonymous said...

Sasa ni dhahiri kuwa mkuu wa nchi kamvika Makonda viatu ambavyo si size yake.Hata hivyo, still kuna room ya Makonda ku- salvage nafasi yake before it gets too late.Anapaswa kuacha kutoa matamko ya kukurupuka,anapaswa kufanya deep consultation kabla ya kurukia issues.vilevile aache kuongoza kuongoza mkoa kibongo fleva kwa kila jambo anataka lionekane kwenye media.