Advertisements

Friday, July 29, 2016

NAIBU WAZIRI HAMAD MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI NCHINI

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia meza kuu ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Kikao hicho, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dk. Zakaria Mganilwa (kulia) alipokuwa anachangia mawazo katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia meza kuu ni Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika kikao cha Baraza hilo cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza kuu) akimsikiliza Katibu wa Baraza hilo ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga (kulia meza kuu) alipokuwa akizungumza katika Kikao cha kujadili Mkakati wa Kupunguza Ajali nchini. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

1 comment:

Anonymous said...

UShauri wangu kwa waziri ni huu ambao kama ataufuata ajali zote zitakwisha mara moja. Pitisha sheria kuwa kama gari litapata jali na uzembe ni wa dereva basi kila abiria ambae amakufa familia yake ilipwe shs. 15,000,000 aliyeumia kwa kukatwa mguu au mkono au kupata kilema chochote alipwe shs. 10,000,000 na aliyepata majeraha yoyote madogo madogo alipwe shs.5,000,000.Halafu dereva aliyesababisha ajali afungiwe leseni ya kuendesha kwa miaka 10.Hii itasadia sana kwa wenye magari kuweza kuwabana madereva wao kuwa makini kwani wataogopa kupata hasara kubwa.History inaeleza ukitaka sheria yoyte ile ifuatwe wabane wenye mali kwenye pesa.Nakuomba waziri kama kweli unataka kumaliza hili tatizo fanya hayo hapo halafu utaona jinsi madereva wakavyokuwa na adabu barabarani.Pia ninayo mawazo mengi kuhusu hili ukitaka wasiliana na mimi hapa halafu tutawasiliana.Asante.