Advertisements

Saturday, July 2, 2016

TAMKO LA RC MAKONDA KUHUSU MASHOGA WALIOPO JIJINI DAR ES SALAAM

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametangaza vita na makaka poa (mashoga) na madada poa (makahaba) walioko jijini Dar es Salaam kuwa utaendeshwa msako mkali wa kuwaondoa.

Mkuu wa Mkoa huyo aliyasema hayo kufuatia hali ya vitendo hivyo visiyokubalika na jamii kuzidi kushamiri na kuwa kuna hatari kubwa ya watoto wadogo kuiga vitendo hivyo vinavyoleta picha mbaya kwani ni kinyume na maadili ya mtanzania.

Aidha alisema hawezi kuifumbia macho hali hii kwani inamomonyoa maadali ya jamii na kuwa yuko tayari kulivalia njuga suala hili ili kuhakikisha anawamaliza wote mkoani
Sakati hili la ushoga na ukahaba limeibuka siku za hivi karibuni baada ya kituo cha televisheni cha Clouds Tv kumhoji shoga mmoja ambapo jamii ilipinga kitendo hicho na kuona kama walikuwa wakiuhalalisha ushoga na kuaminisha jamii kuwa ni kitu kizuri.

4 comments:

Anonymous said...

Mdogo wangu Makonda .....hata kama utapenda tukuchangie dollar mojamoja tutafanya hivyo.ni aibu kuona ushamba wakuiga umetawala ktk familia za Kitanzania (Africa in general)..tena usingetangaza...ungekula nao taratibu.hatuitaji maombi,bali tunatakiwa kukaza buti.

Anonymous said...

Nakubaliana na muheshimiwa Makonda 100% haya mambo ya ushoga sio culture yetu jamani na tusiige mambo ya nchi nyingine na pia itapunguza kuambukiza magonjww ya ukimwi

Anonymous said...
Makonda hana sifa ya kuwa kiongozi wa jamii achilia familia yake! KAMA MTU ALIWEZA KUMPIGA MTU SAWA NA BABA YAKE ALIKUWA AMBAYE WAZIRI MKUU(RTD) JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA anaweza kweli kuwa na sifa ya kuwa DC au RC???Jibu ni the BIG NO.Tumeshuhudia kila siku anavimbishwa kwa sifa za kijinga toka kwa mkuu wa kaya ati ni mchapa kazi.....!!!!Kazi gani hasa anazofanya? Hizi za kuzalilisha akina Mzee Warioba na kutukana Wapinzani???Nonsense.

Mtu unaongea kwa jeuri kabisa ati mkwenye MKOA WANGU WA DAR......! Tangu lini RC akawa na mkoa wake? HIZI NI LUGHA ZA JEURI,KIBURI NA DHARAU kwa watu uliopewa dhamana ya kuwaongoza!!!Haiwezekani kwenye NCHI MOJA KILA MKOA UKAWA NA POLICY/SERA ZAKE KWA MASWALA MAZITO KAMA HAYA YA USHOGA!!!Ushoga ni swala la kitaifa na kimataifa huwezi tu kuweka sheria za kimkoa na ukajiona iumefanya kazi ya kujisifia. Ni upuuzi.

Makonda kama ana akili anatakiwa aangalia SHERIA ZA NCHI ZINASEMA NINI KUHUSU USHOGA ILI KUWA NA SERA MOJA KWA MIKOA YOTE NA HATIMAYE KWA NCHI NZIMA!!Tatizo la nchi hii hata MEDIA zinashindwa kuwauliza MASWALI MAGUMU (HARD TALK)hawa viongozi wanaokurupuka wakiwa hawana vision yoyote kichwani isipokuwa kutaka umaarufu wa kijinga!!
Media mwulizeni Makonda hicho anachokisema kinatekelezeka?? Kama kina tekelezeka kwanini asimshauri mteuzi wake akalipeleka hilo kwenye Cabinet ili kama Serikali waje na lugha moja kwa maana ya sera moja? Hivi leo Makonda akitumbuliwa au kuhamishwa hicho anachokisema kwa Dar kitaendelea au huko atakakohamia ataanzisha sera hiyo???

Sheria zinasemaje mtu akikamatwa anafanya mapenzi ya jinsia moja? Afungwe miaka mingapi au alipe faini kiasi gani? Kumbuka mapenzi ya jinsia moja ni watu wawili wa jinsia moja wanakubaliana kufanya tendo hilo kwenye eneo la siri iwe chumbani hotelini au nyumbani kwao wewe utawakamata vipi na kwa ushahidi upi??
Waandishi wetu wa habari ulizeni maswali kama hayo. Sio kuwaachia viongozi kama hawa waliolewa madaraka wakitoa matamko yenye utata na ubabaishaji!!!

Anonymous said...

Of late Makonda amekuwa mtu wa matamko mengi, lakini implementation ya matamko hayo umekuwa next to nil.Better learn how to put a sizable amount in your mouth that you can chew!
Kwa ugumu wa mkoa huu it is just a matter of time kabla hatujaona bendera nyeupe.