Advertisements

Monday, July 4, 2016

UFARANSA YAFANYA MAUAJI MAKUBWA NA KUTINGA NUSU FAINALI

Nchi ya Ufaransa imeichakaza bila ya huruma Iceland na kumaliza ndoto za taifa hilo kufanya miujiza katika michuano ya Euro 2016 kwa kuifunga magoli 5-2 huko Marseille na sasa watavaana na Ujerumani Alhamisi.

Ushindi huo ulikuwa wa kushtua na uliwafanya mashabiki wa wenyeji Ufaransa wakiwa hawaamini macho yao katika dimba la Stade de France pale walipokuwa kuwa wakiongoza kwa magoli 4-0 hadi mapumziko.

Shuti la chini la Olivier Giroud na kichwa cha nguvu cha Paul Pogba akiunganisha mpira wa kona vilitosha kuwafanya Ufaransa waongoze kwa magoli mawili, kisha Dimitri Payet alifunga goli la tatu na Antoine Griezmann akafunga la nne.


Iceland ilizinduka katika kipindi cha pili pale Kolbeinn Sigthorsson alipounganisha kona ya Gylfi Sigurdsson na kuandika goli la kwanza, kabla ya Oliver Giroud kufunga goli la tano kwa Ufaransa, huku Birkir Bjarnason akifunga goli la pili la Iceland.
 Paul Pogba akiwa juu baada ya kupiga kichwa cha nguvu kilichojaa wavuni
Dimitri Payet akiangalia shuti lake aliloachia na kujaa wavuni
    Mashabiki wa Ufaransa wakishangilia kwa nguvu ushindi

No comments: