Advertisements

Tuesday, August 23, 2016

AJALI GARI LA MAGAZETI YAUA WATANO

Watu watano wamefariki duni kati yao wanne wamekufa papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Noah lililokuwa limebeba magazeti kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania.
Ajali hiyo imetokea leo saa 10:45 alfajiri katika eneo la Alkachenje katika kijiji cha Makanya wilayani Same baada ya gari hilo lililobeba magazeti ya kampuni ya New Habari kugongana na lori hilo.
Gari hilo aina ya Toyota Noah ilikuwa ikitokea Jijini Dar Es Salaam kuelekea Moshi na Arusha wakati lori hilo aina ya Scania ilikuwa ikitokea Arusha kwenda Dar.
Mkuu wa wilaya ya Same,Rosemary Staki ameliambia gazeti hili leo kuwa, abiria wanne walikufa papo hapo na mmoja akafia hospitali ya wilaya ya Same wakati madaktari wakijitahidi kuokoa maisha yake.

No comments: