Advertisements

Tuesday, August 2, 2016

DIAMOND ASEMA ZARI ATAJIFUNGUA MWEZI DISEMBA

Mkali wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari.
Muimbaji huyo amesema yeye na mpenzi wake Zari wanategemea mtoto wa kiume.
“Yah kweli mimi ni baba kijacho,” Diamond alikiambia kipindi cha Leo Tena “Natarajia Mama Tiffa anipatie tena mtoto mwingine, atakuwa wa kiume,”
Aliongeza, “Na itakuwa mwezi Disemba mwaka huu! Baada ya hapo sitaongeza tena mtoto mwingine, ni muda wa kula bata sasa ndio unafata na watoto wetu wawili”
Diamond na Zari tayari wana mtoto mmoja wa kike, ‘Tiffa’ ambaye hivi karibuni atatimiza mwaka mmoja.

3 comments:

Anonymous said...

Is it supposed to be a public notice at all ?

Anonymous said...

Mdau hapo juu kumbuka hawa ni celebrities so have a sit please,congratulations baba na mama T

Anonymous said...

Annon namba moja hapo juu yale yale ya roho mbaya za ndugu wetu wengine wa bongo.