Advertisements

Saturday, August 27, 2016

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LATOA WITO KWA WANANCHI

 KUMEKUWA NA DHANA POTOFU KWA WANANCHI KUWA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI HUFIKA KWA KUCHELEWA KWENYE MATUKIO, KAULI HII SI KWELI BALI JESHI LA ZIMAMOTO HUFIKA KWENYE MATUKIO KWA WAKATI LICHA YA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI

Kuchelewa kufika kwenye tukio husababishwa na mambo yafuatayo:-

(i) Wananchi hususani wanaokuwepo eneo la tukio kuchelewa kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutokana na kuanza kwanza kuokoa mali zilizomo ndani ya Jengo linaloungua bila kutoa taarifa kwanza kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
(ii) Msongamano wa Magari barabarani, pia madereva kutopisha magari ya Zimamoto yanapokuwa yanakwenda kwenye tukio.


(iii) Umbali kutoka vituo vya Zimamoto hadi maeneo ya pembezoni mwa Miji.
(iv) Ujenzi holela nauwekwaji wa vikwazo kama vile matairi chakavu, vyuma na mawe makubwa kando ya mitaa finyu ya maeneo hayo.
(v) Kutoku wepo kwa majina ya mitaa katika maeneo mapya yaliyopimwa na yasiyopimwa.

Mbali ya changamoto zote hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekuwalikiitikia na kutoa magari ndani ya dakika mbili tokea wito ulipo pokelewa. 
WITO KWA WANANCHI:- JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA PINDI WANAPOPATWA NA MAJANGA KAMA VILE MOTO, MAFURIKO, AJARI ZA BARABARANI NA MAJANGA MENGINEYO KWA KUPIGA SIMU YA DHARURA 114 KABLA TUKIO HALIJALETA MADHARA MAKUBWA.

No comments: