Advertisements

Friday, August 12, 2016

MACHOMANE CHAKECHAKE, PEMBA YATEKETEA KWA MOTO

Nyumba inayomilikiwa na Ndg.Salum Said ambaye ni mfanyakazi wa shirika la Umeme Zanzibar ZECO, Tawi la Pemba ikiwa imeteketea yote kwa moto usiku wa kuamkia 
leo Agosti 7,ilioko katika mtaa wa Makondeko Machomanne Chake Chake Pemba, na kusababisha hasara kwa kuungua kwa vitu vyo viliokuwemo katika nyumba hiyo kuteketea kwa moto.Katika ajali hiyo ya moto kwa mujibu wa mashuhuda wanasema hakuna mtu aliyejeruhiwa na ajali hiyo ya moto iliotokea katika majira ya saa sita usiku 
BAADHI ya Nguo za wanafamilia ya Salum Sadi, zikimalizika kuteketea kwa moto baada ya nyumba yake kuungua moto yote, huku vitu vyote vikiwaka, pichani nguo zikimazika kuwaka moto.
Wananchi mbali mbali wakikagua upande wa nyumba ya Salum Sadi, ulioanguka kufuatia juhudi za kuuzima moto ulioteketeza nyumba hiyo usitapakae na kuathiri nyumba nyengine za jirani
MABAKI ya Vitu mbali mbali vilivyopatikana baada ya kuteketea kwa moto, nyumba ya Salum Said huko Makondeko Machomanne Chake Chake Pemba,usiku wa kuamia Agosti 7
 mwaka huu.(Picha na Abdi Suleiman,PEMBA.)

No comments: