Advertisements

Sunday, August 14, 2016

MBINU ZILIZOTUMIKA KUSUKA UKUTA WA CHADEMA

Kama Chadema wana mikakati inayoisumbua CCM; inayoisumbua Serikali au inayovisumbua vyama vingine vya siasa, basi kuna mtu nyuma ya pazia anayebuni na kuratibu mipango hiyo.
Mbinu tofauti zilizotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu zilizofanya wapinzani waweke ushindani wa kihistoria, mbinu zinazotumika wakati likitokea sakata lolote bungeni na mkakati uliotangazwa hivi karibuni wa kupambana na kile kinachodaiwa kuwa ni ukandamizaji wa demokrasia na kupinga ukiukwaji wa sheria, ni mambo yanayokifanya chama hicho kiendelee kuwa midomoni mwa wananchi.
Si mwenyekiti Freeman Mbowe, mwanasheria mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu wala kiongozi mwingine yeyote anayebuni mipango hiyo peke yake bila ya kumshirikisha ‘mchawi’ huyo.
Ni John Mrema; yule kada aliyekuwa anaendesha mikutano yote ya kampeni za urais za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ndiye mchawi wa mikakati ya Chadema kwa sasa ndani na nje ya Bunge.
Ingawa mgombea wa CCM, John Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata kura milioni 8.8, Mrema anaweza kuwa alichangia sehemu kubwa iliyomuwezesha Edward Lowassa kuweka rekodi ya wagombea wa upinzani kwa kupata kura milioni 6.07, takriban mara mbili ya kura walizokuwa wakipata wagombea urais wa upinzani.
Mrema ni kada wa Chadema ambaye alikuwa meneja wa kampeni za urais za Lowassa, ambayo iliundwa na CUF, NCCR-Mageuzi, NLD na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Ndani ya Chadema, Mrema sasa ni mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano, uenezi na mambo ya nje na kabla ya kupewa cheo hicho, alikuwa mkurugenzi wa masuala ya Bunge na Halmashauri.
“Mimi si mchawi, lakini habari za Chadema hazikauki kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari. Nataka muende wenyewe mkafanye utafiti muone jinsi Chadema inavyotawala kwenye mitandao ya kijamii,” alisema Mrema katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika Ijumaa iliyopita.
“Kazi kubwa tunayofanya ni kuangalia hali ya kisiasa na kuamua kipi kifanyike na wakati upi. Ikiwa ndani ya Bunge unaangalia kuna hoja gani na muibue jambo gani.
“Mimi si intelijensia ya Chadema, bali ninachofanya ni kuibua hoja na kutengeneza ‘issue’ (kadhaa za kibunge ambazo wabunge hutumia kupambana na Serikali.”
Chadema imekuwa ikitumia mbinu tofauti kuhakikisha jina la chama linaendelea kung’aa. Wakati wa Bunge la Katiba, chama hicho na vingine vitatu, vilisusia vikao kwa maelezo kuwa chombo hicho kiliachana na Rasimu ya Katiba iliyotokana na maoni ya wananchi na kuingiza ajenda ya CCM na baadaye kuunda Ukawa.
Wakati wa sakata la uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, chama hicho na vingine vya upinzani vilibadili mbinu. Badala ya kususia vikao, wabunge walisimama ndani ya Bunge kupiga kelele kukwamisha shughuli kuendelea hadi matakwa yao yaliposikilizwa.
Lakini baada ya uongozi wa Bunge kuanza kutumia nguvu ya dola kuwaondoa ukumbini, wabunge wa chama hicho na vingine, sasa wanaingia na mbinu tofauti; wanabeba mabango yenye ujumbe, kususia vikao vinavyoongozwa na Naibu Spika mara baada ya sala ya asubuhi, kuziba midomo au kuvaa nguo nyeusi kufikisha ujumbe wao kwa wananchi.
“Ukiwa mkurugenzi wa Bunge wa chama, lazima uwafanye wabunge wote wawe katika himaya yako,” alisema wakati akizungumzia jinsi Chadema inavyoweka mikakati yake bungeni.
“Na lazima uzipitie hoja zao kabla

CHANZO: MWANANCHI

No comments: